51. Hekima ya saba ya swawm: Kuifanya miembamba mishipa

Miongoni mwa hekima za swawm ni kwamba mishipa inakuwa miembamba kwa sababu ya njaa na kiu. Matokeo yake njia za shaytwaan mwilini zinakuwa nyembamba. Kwani hakika shaytwaan hutembea ndani ya mwanadamu kama ambavo damu inatembea, kama ambavo hayo yamethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo wasiwasi wa shaytwaan unapata kutulia na nguvu za matamanio na hasira zinavunjika. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la mabarobaro! Yule miongoni mwenu atakayeweza kuoa basi na aoe. Kwani hilo litamfanya kuteremsha macho zaidi na kuhidhi utupu. Asiyeweza basi afunge. Kwani hiyo kwake ni kinga.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Akafanya funga kuwa ni kinga ya matamanio ya tendo la ndoa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 66
  • Imechapishwa: 13/04/2021