50. Tukate swawm tukiwa angani ilihali tunaona jua au tusubiri ndege ituwe?

Swali 50: Ndege itatupaisha kwa idhini ya Allaah kutoka Riyaadh katika Ramadhaan takriban saa moja kabla ya adhaana ya Maghrib na wataadhini kwa ajili ya Maghrib tukiwa kwenye anga ya Saudi Arabia. Je, tukate swawm? Tukiona jua ilihali tuko angani – kama inavokuwa mara nyingi – tuendelee kufunga na kukata swawm katika nchi yetu au tukate swawm kwa kule kusikia adhaana Saudi Arabia[1]?

Jibu: Ndege ikipaa kutoka Riyaadh kwa mfano kabla ya kuzama kwa jua upande wa magharibi, basi unaendelea kuwa mfungaji mpaka jua lizame ilihali uko angani au umeshashuka katika nchi ambayo jua limekwishazama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukija hapa [mashariki] na ukaondoka mchana hapa [magharibi] na likazama jua, basi amekwishafungua mfungaji.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/322-323).

[2] al-Bukhaariy (1954) na Muslim (1100 na 1101).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 67
  • Imechapishwa: 20/05/2022