Muhammad bin Idriys ash-Shaafi´iy al-Matwalabiy, imamu aliyetangulia, bwana mwenye kutukuzwa, neema kubwa juu ya Uislamu na waislamu, muwafikishwaji, mwenye kupewa ilhamu, mwenye kufanywa imara, ambaye aliifanyia kazi dini ya Allaah na Sunnah zake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye hana mfano katika wanazuoni waliokuwa wakiishi katika zama zake na waliokuwa baada yake inapokuja katika kuinusuru na kuitetea.

Miongoni mwao wako ambao walikuwa wakiishi kabla ya ash-Shaafi´iy kama Sa´iyd bin Jubayr, az-Zuhriy, ash-Sha´biy na at-Taymiy.

Baada yao akaja al-Layth bin Sa´d, al-Awzaa´iy, ath-Thawriy, Sufyaan bin ´Uyaynah al-Hilaaliy, Hammaad bin Salamah, Hammaad bin Zayd, Yuunus bin ´Ubayd, Ayyuub, Ibn ´Awn na wenzao.

Baada yao akaja mfano wa Yaziyd bin Haaruun, ´Abdur-Razzaaq, Jariyr bin ´Abdil-Hamiyd.

Baada yao akaja mfano wa Muhammad bin Yahyaa adh-Dhuhliy, Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy, Muslim bin al-Hajjaaj al-Qushayriy, Abu Daawuud as-Sijistaaniy, Abu Zur´ah ar-Raaziy, Abu Haatim na mtoto wake, Muhammad bin Muslim bin Waarah, Muhammad bin Aslam at-Twusiy, ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy, Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah – ambaye pia alikuwa akitambulika kama imamu wa maimamu, na naapa kwa Allaah ya kwamba alikuwa imamu wa maimamu katika zama zake – Abu Ya´quub Ishaaq bin Ismaa´iyl al-Bustiy, babu yangu Abu Sa´iyd Yahyaa bin Mansuur al-Harawiy az-Zaahid, ´Adiy bin Hamduuyah as-Swaabuuniy, watoto wake wawili na upanga wa Uislamu Abu ´Abdillaah as-Swaabuuniy na Abu ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy na wengine katika maimamu wa Sunnah ambao walikuwa wameshikana nayo barabara, wakiinusuru, wakilingania kwayo na wakielekeza kwayo.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 310-315
  • Imechapishwa: 01/01/2024