51. Mtazamo wenye maafikiano kwa Ahl-ul-Bid´ah

Sentesi hizi nilizozithibitisha katika kitabu hiki ilikuwa ndio ´Aqiydah ya wote hao. Hakuna yeyote aliyeona kinyuma. Bali wote waliafikiana na yaliyomo ndani. Aidha waliafikiana juu ya kuwashinda Ahl-ul-Bid´ah, kuwatweza, kuwafedhehesha, kuwaepuka na kujitenga nao mbali, kusuhubiana nao na kutangamana nao. Walikuwa wanaona ni kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kule kuwaepuka na kuwakata.

Kutokana na fadhilah za Allaah mimi ni mwenye kufuata nyayo zao, kuangazwa na nuru zao, nawanasihi ndugu na marafiki zangu kutopinda kutokana na vinara wao, wasifuate maneno ya watu wengine na wasijishughulishe na Bid´ah hizi zilizotangaa, kuenea na kusambaa kati ya waislamu. Lau moja wapo tu ingelitoka kwenye ulimi wa mmoja katika zama za maimamu hao,  basi wangelimkata, wakamtia kwenye Bid´ah, kumuona ni mwongo na kumsibu kwa kila baya na lenye kuchukiza.

Ndugu zangu – Allaah awahifadhi – msighurike na wingi wa Ahl-ul-Bid´ah na idadi yao kubwa, kwa sababu hilo si jengine isipokuwa tu ni alama ya kukaribia Qiyaamah. Mtume mteule amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Miongoni mwa alama za Saa na kukaribia kwake ni elimu kuwa chache na ujinga kuwa mwingi.”

Elimu ni Sunnah na ujinga ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 315-316
  • Imechapishwa: 01/01/2024