Moja katika alama za Ahl-us-Sunnah ni kuwapenda maimamu wa Sunnah, wanazuoni, wanusuraji na wapenzi wake na kuwachukia viongozi wa Bid´ah ambao wanalingania katika Moto na wanawavuta wafuasi wao Motoni. Allaah (Ta´ala) amezipamba na kuziangaza nyoyo za Ahl-us-Sunnah kuwapenda wanazuoni wa Sunnah – fadhilah na neema kutoka kwa Allaah.

al-Haakim Abu ´Abdillaah al-Haafidhw – Allaah amjaze yeye na sisi Peponi – ametukhabarisha: Muhammad bin Ibraahiym bin al-Fadhwl al-Muzakkaa ametuhadithia: Ahmad bin Salamah ametuhadithia: Abu Rajaa’ Qutaybah bin Sa´iyd ametusomea kitabu ”Kitaab-ul-Iymaan” ambacho ni chake. Imekuja mwishoni mwake:

”Ukimuona mtu anampenda Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, al-Awzaa´iy, Shu´bah, Ibn-ul-Mubaarak, Abul-Ahwasw, Shariyk, Wakiy´, Yahyaa bin Sa´iyd na ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, basi utambue kuwa ni mtu wa Sunnah.”

Ahmad bin Salamah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Chini yake nikaweka hati yangu mwenyewe ya mkono: Na Yahyaa Ahmad bin Hanbal na Ishaaq bin Raahuuyah.”

Wakati alipofika katika maudhui haya wakatutazama watu wa Naysaabuur na kusema: ”Watu hawa wanamchukia Yahyaa bin Yahyaa.” Tukamwambia: ”Ee Abu Rajaa´, ni nani Yahyaa bin Yahyaa?” Akasema: ”Ni mtu mwema, imamu wa waislamu. Ishaaq bin Ibraahiym pia ni imamu. Ahmad bin Hanbal ni mkubwa zaidi kuliko hao wote niliyokutajia.”

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 307-310
  • Imechapishwa: 01/01/2024