Ahl-us-Sunnah vilevile wako kati kwa kati inapokuja katika matendo ya Allaah, baina ya Wa´iydiyyah na Qadariyyah. Wanathibitisha matendo ya Allaah na kwamba ni haki. Yeye (Jalla wa ´Alaa) hushuka katika mbingu ya chini kila usiku, atajionyesha kwa waja Wake siku ya Qiyaamah ili waweze kuona uso Wake mtukufu kama unavyoonekana mwezi waziwazi pasi na kuwepo mawingu (Subhaanahu wa Ta´ala). Huridhia, hughadhibika, huamrisha, hukataza, huumba na huruzuku. Matendo Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) ni kitu kimethibiti. Tofauti na wakanushaji ambao ni Jahmiyyah. Mu´tazilah wanasema kuwa inatakiwa kuthibitisha majina na si sifa. Wanasema kuwa eti majina ya Allaah yathibitishwe matupu bila ya maana.
Ahl-us-Sunnah wako kati kwa kati baina ya Wa´iydiyyah ambao wanasema kuwa matishio ya Allaah ni lazima yatekelezwe. Murji-ah wenye kuyaondosha matendo [katika imani] na wanaonelea kuwa mja anachotakiwa ni kutamka na kuamini pasi na kuleta matendo kwa kuwa sio katika imani. Wa´iydiyyah ambao ni Mu´tazilah wao wanategemea makemeo ya Allaah na wasema kuwa mtenda dhambi kubwa atadumishwa Motoni milele endapo atakufa juu ya maasi. Upande mwingine wa Murji-ah wao wanasema kuwa hakuna kitu chenye kuidhuru imani kwa sababu wanaona kuwa matendo hayaingii katika imani. Wanaonelea inatosha mtu akitamka na kusadikisha.
Ahl-us-Sunnah wao wanaonelea kuwa imani ni kutamka, kuleta matendo na kuamini na vilevile maasi yanaidhuru imani. Lakini hata hivyo hayapelekei kudumishwa Motoni milele, kama wanavyosema Mu´tazilah. Kadhalika hayamfanyi mtu akakufuru, kama wanavyosema Khawaarij. Lakini maasi yanaidhuru na kuidhoofisha. Kuachana na maasi na kutubia kwayo kunaifanya imani kuwa kamilifu.
Ahl-us-Sunnah wako kati kwa kati baina ya Wa´iydiyyah (Mu´tazilah na Khawaarij) na Murji-ah. Khawaarij wanasema imani ni kutamka, kufanya matendo na kuamini, lakini haizidi na wala haipungui. Vilevile Wa´iydiyyah wakiwemo Mu´tazilah wanasema kuwa imani ni kutamka, kufanya matendo na kuamini, lakini haizidi na wala haipungui. Mwenye kufa juu ya maasi anakuwa ni miongoni mwa watu wa Motoni na atadumishwa humo milele. Khawaarij wametofautinaa na Mu´tazilah kwa kuona kuwa ni kafiri na wakati huohuo ni katika watu wa Motoni.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 70-72
- Imechapishwa: 24/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)