Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) sade:
Hakika kundi lililookoka, Ahl-usSunnah wal-Jamaa´ah, wanaamini hayo kama jinsi wanavyoamini Aliyojielezea Allaah katika Kitabu Chake, bila ya kupotosha, kupindisha maana, kuyafanyia namna wala kufananisha.
Bali wao wako kati kwa kati baina ya mapote ya ummah, kama jinsi ummah ulivyo kati kwa kati baina ya nyumati zingine.
Wako kati kwa kati katika mlango wa sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), baina ya wanaokanusha Jahmiyyah na wanaofananisha Mushabbihah.
Wako kati kwa kati katika mlango wa matendo ya Allaah (Ta´ala), baina ya Qadariyyah, Jabriyyah na wengineo.
Hali kadhalika katika mlango wa tishio la Allaah, baina ya Murji-ah na Wa´iydiyyah miongoni mwa Qadariyyah na wengineo.
Vivyo hivyo kuhusiana na imani na dini ni kitu gani, baina ya Haruuriyyah na Mu´tazilah, Murji-ah na Jahmiyyah.
Hali kadhalika kuhusiana na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam), kati ya Rawaafidhw na Khawaarij.
MAELEZO
´Aqiydah ya Ahl-usSunnah wal-Jamaa´ah ni ´Aqiydah iliyonyooka sawasawa na ilio kati kwa kati katika mlango huu na mingine. Wako kati kwa kati kuhusiana na Allaah. Kama ambavyo ummah huu uko kati kwa kati baina ya nyumati zingine basi Ahl-us-Sunnah wako kati kwa kati katika mlango huu pale ambapo wanamthibitishia Allaah sifa na majina Yake pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuziwekea namna wala kuzilinganisha. Kwa msemo mwingine wanazipitisha kama zilivyokuja na hawazipotoshi, kuzikanusha na kuzilinganisha sifa za Allaah na sifa za viumbe Wake, kama wanavyofanya Jahmiyyah na Mu´tazilah. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wao wanazithibitisha uthibitisho usiokuwa na ufananishaji na wakati huohuo wanamtakasa Allaah kufanana na viumbe Vyake utakaso usiokuuwa na ukanushaji. Uthibitishaji wa sifa na majina ya Allaah hauhitajii kufananisha kama ambavyo utakaso vilevile hauhitajii ukanushaji. Bali wanasema kuwa wao wanamthibitishia Allaah sifa na majina kwa njia inayolingana Naye pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuyawekea namna na kuyafananisha. Wako kati kwa kati inapokuja katika mlango wa sifa na majina ya Allaah, baina ya wakanushaji ambao ni Jahmiyyah na wafananishaji ambao ni Mushabbihah.
Jahmiyyah wanakanusha sifa na majina ya Allaah. Mushabbihah wao wanayathibitisha, lakini pamoja na hivyo wanasema kuwa mkono wa Allaah ni kama mkono wangu, sauti ya Allaah ni kama sauti yangu, mguu wa Allaah ni kama mguu wangu. Wanafananisha sifa za Allaah na za viumbe. Huu ni uovu mkubwa kabisa. Ni kufuru na upotevu. Wako kati kwa kati baina ya wanaokanusha ambao ni Jahmiyyah na wanaofananisha ambao ni Mushabbihah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 70
- Imechapishwa: 24/10/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 70
Imechapishwa: 24/10/2024
https://firqatunnajia.com/48-ahl-us-sunnah-watu-wa-kati-na-kati/