Vilevile kuhusiana na Hadiyth pale ambapo walinyanyua sauti zao akawaambia:
“Enyi watu! Zihurumieni nafsi zenu! Kwani hakika hamumuombi ambaye ni kiziwi wala asiyekuwepo. Hakika Yule mnayemwomba ni Mwenye kusikia Mwenye kuona na Aliye karibu. Hakika yule mnayemwomba Yuko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko shingo ya vipando vyenu.”
Hapa amewabainishia (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ya kwamba Yeye (Subhaanah) anayasikia maneno na du´aa za waja Wake. Kwa hivyo hahitajii mtu kunyanyua sauti inayopingana na Shari´ah. Kunyanyua sauti kunatakiwa iwe kwa wastani. Kwa ajili hii ndipo akasema kuwaambia:
“Hamumuombi ambaye ni kiziwi wala asiyekuwepo.”
Walikuwa ni wenye kunyanyua sauti zao. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamrisha wasifanye hivyo ambapo wanapitiliza katika unyanyuaji juu. Isipokuwa tu wakati wa Talbiyah. Hili ni jambo ambalo limevuliwa. Kuna dalili zenye kuonyesha kuwa inatakiwa kunyanyua sauti ya juu. Lakini Takbiyr ya kawaida inatakiwa iwe kwa sauti ya wastani na isiwe kwa kunyanyua sauti sana. Kwani hamumuombi ambaye ni kiziwi wala asiyekuwepo. Yeye yuko juu ya ´Arshi na wakati huohuo yuko pamoja na waja Wake kwa njia ya kwamba anazisikia sauti na maneno yao (Jalla wa ´Alaa). Amesema (Ta´ala):
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ
“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.” (02:186)
Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika yule mnayemwomba Yuko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko shingo ya vipando vyenu.”
Yeye (Subhaanah) yuko karibu na hahitajii mtu akapindukia kwa sauti wakati wa Dhikr. Aombe kwa sauti ya kusikika kidogo kwa njia ya kumdhukuru Allaah na si kwa njia ya kwamba Allaah anahitajia hilo. Anaponyanyua sauti yake kidogo ni kwa njia ya Dhikr na kudhihirisha kumdhukuru Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ni kama pale ambapo watu wanapodhihirisha sauti zao wakati wa Talbiyah. Lengo ni kudhihirisha kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jall). Vinginevyo ni kwamba Yeye (Subhaanah) anayajua ya siri na yaliyojificha, anasikia sauti za waja hata kama watanong´oneza. Hakuna chochote kinachojificha Kwake. Yeye ni Mwenye kusikia na yukaribu, anazisikia sauti zao hata kama watanong´oneza. Kama ambavyo anazijua hali zao hata kama watazificha. Hakuna chochote kinachojificha Kwake (Jalla wa ´Alaa).
Kwa hivyo ni wajibu kwa muumini kumuamini Allaah na kwamba Yeye (Subhaanah) ni Mwenye kusikia na yukaribu, anajua hali za waja Wake, anasikia sauti zao na anajua maombi yao na hakuna chochote chenye kujificha Kwake (Jalla wa ´Alaa) pamoja na kuwa kwa wakati huohuo yuko juu ya ´Arshi na juu ya viumbe wote (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni tofauti na ´Aqiydah ya Ahl-ul-Bid´ah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 69-70
- Imechapishwa: 24/10/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 69-70
Imechapishwa: 24/10/2024
https://firqatunnajia.com/47-allaah-yuko-karibu-na-waja-wake/