Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Jua ya kwamba hoja tata hizi tatu ndio kubwa walizonazo. Ukishajua kuwa Allaah katuwekea nazo wazi katika Kitabu Chake na ukazifahamu vizuri, yaliyo baada yake yatakuwa sahali zaidi kuliko hayo.

MAELEZO

Hoja tata ya kwanza: Wanasema kuwa wao hawaabudu masanamu, bali wanaabudu mawalii.

Hoja tata ya pili: Wanasema kuwa wao hawawakusudii wao bali wanayemkusudia kumuabudu ni Allaah (´Azza wa Jall) pekee.

Hoja tata ya tatu: Wanasema kuwa hawawaabudu ili wawanufaishe au wawadhuru. Manufaa na madhara yako mkononi mwa Allaah (´Azza wa Jall). Wanachokusudia ni wawakurubishe mbele ya Allaah. Hivyo eti hii sio shirki.

Ikikubainikia namna ya kuzifichua hoja tata hizi, basi hoja tata zenye kuja baada ya hizi ni sahali kuzifichua na kuzivunja, kwa sababu hizi ndio hoja tata wanazibabaisha watu kwazo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 65
  • Imechapishwa: 24/11/2023