48. Washirina katika zama za Mtume pia walikuwa wakiwaomba waungu wao uombezi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ikiwa atasema: “Makafiri walikuwa wanataka [manufaa na madhara] kutoka kwao, na mimi ninashuhudia ya kwamba Allaah ndiye mwenye kunufaisha, mwenye kudhuru na mwendeshaji wa mambo. Sitaki [manufaa na madhara] isipokuwa kutoka Kwake. Na watu wema hawana sehemu yoyote katika hayo. Lakini ninawaomba kwa kuwa natarajia kutoka kwa Allaah uombezi wao.” Jibu ni kuwa, maneno haya na yale ya makafiri ni sawasawa. Msomee maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi [wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.” (39:03)

هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

MAELEZO

Washirikina wanamaanisha kwamba makafiri walikuwa wakiwaabudu moja kwa moja ili waweze kuwanufasha na kuepusha madhara, ilihali yeye anamwelekea Allaah kwa ajili ya hayo. Waja wema hawana sehemu yoyote katika hayo. Haamini kuwa wana lolote, lakini anajikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) ili wawe mwombezi wake.

Mwambie kuwa washirikina ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumilizwa kwao walikuwa wakisema hayohayo. Hawakuabudu masanamu haya kwa kuamini kuwa yalikuwa yakinufaisha na kudhuru. Walikuwa wakiyaabudu ili yaweze kuwakurubisha mbele ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.”

هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”

Hivyo hali yake na hali ya washirikina hawa zinaenda sambamba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 64