Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwa hivyo batili hii ikawa imejengwa juu ya kuharibika kwa akili na kukufuru Wahy. Hakika si vyenginevyo wameegemea mambo ya kiakili, ambayo wamedhani kuwa ni hoja za wazi ilihali ukweli wa mambo ni kwamba si chochote isipokuwa tu hoja tata, na wakayakengeusha maandiko kuyaondoa mahali pake stahiki.
MAELEZO
Katika kumkanushia Allaah sifa wametegemea kanuni za mantiki na falsafa. Wanazingatia vitu hivyo kuwa ni dalili za kiakili na za yakini, ilihali dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah wanazizingatia kuwa ni dalili za kudhania tu. Ndio wanaitanguliza mbele akili juu ya Qur-aan na Sunnah. Ukweli wa mambo ni kinyume chake; mantiki ni jambo la kudhaniwa, nyingi katika mambo hayo ni ujinga na upotofu mtupu. Sambamba na hilo Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anasema juu ya Qur-aan:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيد
“Haiingiliwi na batili mbele na nyuma yake – ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[1]
الر كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ
“Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[2]
Qur-aan ndio ya kukata kabisa na yenye yakini, kwa sababu ni maneno kutoka kwa Mwingi wa hekima, Anayestahiki kuhimidiwa.
Kuhusu mantiki ni yenye kutoka kwa mwanadamu; utangulizi, matokeo, dutu, isiyo ya kimwili, kiwiliwili na mfano wa hayo. Ni mambo tu ya kudhania na ujinga. Wamekuja na mambo haya na kuyafanya kuwa ndio marejeo yanayorejelewa katika Tawhiyd. Matokeo yake wakapotea wao na kuwapotosha wengine. Ni kanuni mbaya kwa vile wameweka nafasi ya Qur-aan na Sunnah mantiki na falsafa. Mambo yanatakiwa kuwa kinyume na hivo. Mategemeo inatakiwa iwe Qur-aan na Sunnah na kuachana na mijadala na mantiki. Wakati wa al-Ma´muun falsafa ya kigiriki ilifanyiwa tarjama kwa kiarabu na hapo ndipo waislamu waliingiliwa na mantiki, mijadala na falsafa. Kuhusu Qur-aan ni yenye kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Sunnah ni yenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kutoka kwa Allaah. Kuna tofauti kati ya vyanzo hivo viwili; moja inatoka kwa wagiriki na nyingine ambayo ni Qur-aan ni yenye kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) na Sunnah.
[1] 41:42
[2] 14:01
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 80-81
- Imechapishwa: 12/08/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 80-81
Imechapishwa: 12/08/2024
https://firqatunnajia.com/49-mantiki-na-falsafa-badala-ya-qur-aan-na-sunnah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)