16 – Imependekezwa kwa mwanamke kutembelea msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya kuswali na kuomba du´aa ndani yake. Lakini haijuzu kwake kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu amekatazwa kutembelea makaburi. Shaykh Muhammad bin Ibrahiym Aalush-Shaykh (Rahimahu Allaah), ambaye alikuwa Muftiy wa Saudi Arabia, amesema katika “Majmuu´-ul-Fatawaa”:

“Maoni sahihi katika masuala haya ni kwamba mwanamke amekatazwa kulitembelea kaburi lake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ya maambo mawili:

1 – Ueneaji wa dalili na makatazo yakitajwa kwa ujumla basi haijuzu kwa yeyote kuyafanya maalum isipokuwa kwa dalili.

2 – Jengine ni kwamba sababu imepatikana hapa.”[1]

Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Hafidhwahu Allaah) amesema katika “al-Mansik” yake, wakati alipotaja kuhusu kulitembelea kaburi lake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yule aliyetembelea msikiti wake mtukufu, akasema:

“Matembezi haya ya kaburi lake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa yule aliyetembelea msikiti wake mtukufu; kisha akasema: “Matembezi haya yamesuniwa kwa wanaume peke yao. Ama wanawake haifai kwao kutembelea kaburi lolote, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyafanya ni pahali pa kuswalia na wenye kuyatia mataa. Ama kukusudia al-Madiynah kwa ajili ya kuswali ndani ya msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuomba du´aa ndani yake na mfano wa hayo ambayo yamesuniwa pia katika misikiti mingine ni jambo limesuniwa kwa wote.”

[1] (03/239).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 96
  • Imechapishwa: 18/11/2019