Amesema (Ta´ala) kuhusu wakazi wa Motoni:

وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا

”Na wale waliokufuru watapata Moto wa Jahannam; hawatahukumiwa kifo wakafa na wala hawatawepesishiwa adhabu yake.”[1]

أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

”… hao wamekata tamaa na rehema Yangu na hao watapata adhabu iumizayo.”[2]

أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ

”Je, hawa si ni wale ambao mliapa kwamba Allaah hatowapa rehema yoyote ile?”[3]

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ

“Wataita: “Ee Maalik! Atumalize tufe Mola wako!” Atasema: “Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo!”[4]

سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ

”Ni sawasawa kwetu tukitia shaka au tukisubiri; hatuna mahali pa kukimbilia!”[5]

خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ

”… ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu wa viumbe.”[6]

كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ

”… kila ngozi zao zitakapobanikika zikachomeka Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje vyema adhabu.”[7]

كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ

”Kila watakapotaka kutoka humo kwa sababu ya dhiki, watarudishwa humo na [kuambiwa]: ”Onjeni adhabu ya kuchomeka!”[8]

إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ

”… hakika huo ni wenye kufungwa juu yao kila upande.”[9]

Mifano kama hiyo ndani ya Qur-aan ni mingi[10].

[1] 35:36

[2] 29:23

[3] 7:49

[4] 43:77

[5] 14:21

[6] 98:6

[7] 4:56

[8] 22:22

[9] 104:08

[10] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 169-170
  • Imechapishwa: 01/05/2024