Yeyote anayeona kuwa atakuja Nabii mwingine baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kafiri na ametoka nje ya dini. Ameeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba watajitokeza waongo ambao wanadai kuwa ni Manabii na akasema:

“Watakuja baada yangu waongo thelathini na wote watadai kuwa ni Manabii. Hata hivyo mimi ndiye Nabii wa mwisho. Hakuna Nabii mwingine baada yangu.”[1]

Yule atakayedai kuwa ni Nabii, au akadaiwa kuwa ni Nabii na wale watakaowafuata wote ni makafiri. Watu kama hao wamepigwa vita na Uislamu na wakawakufurisha. Mtu wa mwisho ambaye amedai utume ni bwana mmoja muhindi kwa jina Ahmad al-Qaadiyaaniy. Wafuasi wake wanaitwa Qadiyaaniyyah. Wanaweza pia kunasibishwa na jina lake na wakaitwa Ahmadiyyah. Wanazuoni wamemkufurisha yeye na wafuasi wake na wakawafukuza kutoka katika nchi za waislamu. Kwa sababu ´Aqiydah hii maana yake ni kumkadhibisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna muislamu yeyote ambaye ameonelea kinyume juu ya ukafiri wao. Kwa hivyo ni lazima kwa muislamu kuamini kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Nabii, Mtume wa mwisho na kiongozi wa wenye kumcha Allaah. Yeye ndiye ruwaza njema pekee ya wale wenye kumcha Allaah (´Azza wa Jall):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَا

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah kwa yule mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho.”[2]

Kuhusu wengine wote, wanafuatwa pale ambapo wamemfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu anayekwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi haijuzu kumuigiliza:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[3]

Njia pekee ya kumfikia Allaah ni kumfuata na kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Ahmad (22395), Abu Daawuud (4252), at-Tirmidhiy (2219), Ibn Hibbaan (7238) na Abu Nu´aym (2/289). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaat” (5406).

[2] 33:21

[3] 3:31

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 09/12/2022