Ama masimulizi ya Rabiy’ah ar-Ray´, ameyapokea al-Laalakaa’iy katika “Sharh Usuwl I’tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa’ah” na Ibn Qudaamah katika “Ithbaat-ul-‘Uluww” kupitia kwa Yahyaa bin Aadam, kutoka kwa Ibn ´Uyaynah, ambaye amesema:
“Rabiy’ah aliulizwa kuhusu maneno Yake (Ta’ala):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
Amelingana juu vipi?” Akajibu: ”Kulingana juu si kitu kisichojulikana. Namna si kitu kisichofahamika. Ujumbe ni wenye kutoka kwa Allaah, ni juu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kufikisha na ni juu yetu kusadikisha.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema kuhusiana na masimulizi hayo:
“al-Khallaal amepokea kwa cheni ya wasimulizi ambao wote ni madhubuti, kutoka kwa Sufyaan bin ‘Uyaynah, ambaye amesema:
“Rabiy’ah bin Abiy ‘Abdir-Rahman aliulizwa kuhusiana na maneno Yake (Ta’ala)…”[2]
adh-Dhahabiy ameipokea katika “al-‘Uluww” kupitia kwa an-Najaad: Mu’aadh bin al-Muthannaa ametuhadithia: Muhammad bin Bishr amenihadithia: Sufyaan (ath-Thawriy) ametuhadithia:
“Nilikuwa kwa Rabiy’ah bin Abiy ‘Abdir-Rahmaan…”[3]
al-Albaaniy amesema kwamba ni Swahiyh[4].
al-Bayhaqiy ameipokea katika “al-Asmaa was-Swifaat” kupitia kwa ´Abdullaah bin Swaalih bin Muslim, ambaye amesema:
“Rabiy’ah ar-Ray’ aliulizwa kuhusiana na maneno yake Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”
Amelingana juu vipi?” Akajibu: ”Namna haitambuliki na Kulingana juu ni kitu kisichofahamika. Ni wajibu kwangu na kwenu kuamini jambo hilo.”[5]
Hata hivyo tamko hili linaenda kinyume na yale mawili yaliyotangulia. Katika cheni ya wapokezi kuna Abu Swaalih ́Abdullaah bin Swaalih bin Muslim al-Miswriy, mwandishi wa al-Layth. Haafidhw Ibn Hajar amesema:
“Ni mkweli mwenye makosa mengi. Alikuwa thabiti wakati anaposimulia kutoka kwenye kitabu chake. Alikuwa na uzembe.”[6]
Zaidi ya hayo ni kwamba hakuwahi kukutana na Rabiy’ah. Kwa mujibu wa wasifu wake katika “Tahdhiyb-ul-Kamaal” alizaliwa mwaka wa 137, ilihali Rabiy’ah ar-Ray’, kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi, alikufa mwaka wa 136. Hivyo ndivo imekuja katika “Taqriyb-ut-Taqriyb” ya Ibn Hajar.”
[1] 20:05
[2] al-Hamawiyyah, uk. 32.
[3] al-´Uluww, uk. 98.
[4] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 97.
[5] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/306-307).
[6] Taqriyb-ut-Taqriyb.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 69-70
- Imechapishwa: 12/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 69-70
Imechapishwa: 12/12/2025
https://firqatunnajia.com/47-tamko-la-umm-salamah-la-masimulizi-ya-maalik/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket