Swali: Maneno ya Allaah kuhusu wanafiki:
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا
”… isipokuwa wale waliotubu na wakatengeneza na wakashikamana na Allaah na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na waumini; na Allaah atawapa waumini ujira mkubwa kabisa.”[1]
Jibu: Wakitubia basi Allaah anawakubalia. Mlango wa tawbah uko wazi. Akipotoka kisha akatubia basi Allaah anamkubalia. Kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoeleza kwamba tawbah hufuta yaliyotangulia. Alipotaja shirki, uzinzi na mauaj, akasema:

”… isipokuwa wale waliotubu na wakatengeneza na wakashikamana na Allaah na wakaitakasa dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na waumini; na Allaah atawapa waumini ujira mkubwa kabisa.”
Lakini jasusi sivyo. Jasusi tawbah yake haikubaliki. Kwa sababu ikikubaliwa tawbah yake basi majasusi watakuwa wengi na kila wakikamatwa watasema kuwa wametubia. Maslahi yataharibika na balaa itatokea. Jasusi haachiwi, bali huawa, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowaua majasusi. Lakini huyu alikuwa Haatwib tu, kwa sababu alikuwa miongoni mwa watu wa Badr na alidhani kwamba hili halitamdhuru. Kisha Allaah akambainishia jambo hilo baada ya hapo na akabainisha suala hilo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ
“Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki mkiwapelekea mapenzi.”[2]
Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya hapo akaeleza na akaamuru kuuawa kwa jasusi.
[1] 04:146
[2] 60:1
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31688/هل-للمنافق-والجاسوس-توبة
- Imechapishwa: 05/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31688/هل-للمنافق-والجاسوس-توبة
Imechapishwa: 05/12/2025
https://firqatunnajia.com/tawbah-ya-mnafiki-na-jasusi/