47. Mwandishi wa kitabu amewajibu wapinzani wake kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah

Na nitakutajia kitu katika yale aliyotaja Allaah katika Kitabu Chake jibu kwa maneno ambayo washirikina wa zama zetu wanatumia kama hoja dhidi yetu.

MAELEZO

Pindi alipokuletea kanuni hii kubwa inayosema:

“Mtu wa batili hawezi kuja na hoja isipokuwa katika Qur-aan kuna yanayoivunja na kubainisha ubatilifu wake.”

na kusema kwamba hilo ni jambo linaloendelea mpaka siku ya Qiyaamah, ndipo akaingia katika kuleta mifano yaliyompitikia Shaykh (Rahimahu Allaah) katika wakati wake dhidi ya mahasimu zake.

Kuanzia hapa mpaka mwisho wa kitabu ni kufichua utata wanaomletea Shaykh na yeye anawajibu kutoka katika Qur-aan na Sunnah na kuziponda hoja zao. Kwa ajili hiyo Allaah akamnusuru dhidi yao na akabatilisha vitimbi vyao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 65
  • Imechapishwa: 21/12/2016