Mtu akiuliza ni kwa nini shahidi (شهيد) ameitwa hivo, wanachuoni wametofautiana juu ya hilo:

1- Kwa kuwa yuko hai, kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

“Na wala usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Allaah wamekufa. Bali wahai kwa Mola wao wanaruzukiwa.” 03:169

2- Kwa kuwa Allaah na Malaika Wake wameshuhudilia شهدوا Peponi.

3- Kwa kuwa Malaika wanamshuhudilia تشهد .

4- Kwa kuwa ameshuhudia haki تشهادة mpaka akauawa.

5- Kwa kuwa ameshuhudia يشهد yale Allaah aliyomuahidi juu ya karama za kifo.

6- Kwa kuwa ameshuhudia شهد uwepo wa Allaah na haki ya upwekee ya kuabudiwa kwa vitendo wakati wengine wamemshudilia kwa maneno.

7- Kwa kuwa ameanguka kwenye ardhi inayomshuhudilia شاهد .

8- Kwa kuwa anashuhudia شهد ya kwamba ni lazima aingie Peponi.

9- Kwa sababu ya shahidi wake شاهد ambaye ni damu.

10- Kwa kuwa Amemshuhudilia شهد imani na mwisho mwema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 229-230
  • Imechapishwa: 21/12/2016