Swali 47: Kuhusu yale uliyoyataja juu ya kufunga na kufungua pamoja nasi kwa vile mlikaa Uhispania masiku ya Ramadhaan[1].
Jibu: Hapana neno wala vibaya juu yenu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Fungeni kwa kuuona [mwezi] na fungueni kwa kuuona mwezi. Mkifunikwa na mawingu basi kamilisheni idadi ya [siku] thelathini.”[2]
Haya ni yenye kuenea kwa Ummah mzima. Saudi Arabia ndio nchi yenye haki zaidi kufuatwa kwa kujitahidi kwake kuhukumu kwa Shari´ah. Allaah azidi kuafikisha na kuiongoza. Isitoshe nyinyi mko katika nchi ambayo haihukumu kwa Uislamu na wala raia wake hawatilii umuhimu hukumu ya Uislamu.
Kuhusu swali lenu kuhusu kukusanya kati ya swalah mbili jambo lake ni lenye wasaa. Shari´ah safi imefahamisha juu ya kufaa kwake katika wakati wa mwanzo na wa pili au kati ya swalah mbili. Kwa sababu wakati wake umekuwa mmoja kwa haki ya yule ambaye amepewa udhuru kama kwa msafiri na mgonjwa. Vilevile inafaa kuzungumza kati ya swalah mbili zinazokusanywa kwa yale yanayopekea haja.
Kuhusu Witr wakati wake unaanza kuanzia pale mtu anapomaliza kuswali ´Ishaa ijapo ni yenye kukusanywa pamoja na Maghrib katika wakati wa swalah ya Maghrib.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/105-106).
[2] Muslim (1081) na an-Nasaa´iy (2124).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 64-65
- Imechapishwa: 18/05/2022
Swali 47: Kuhusu yale uliyoyataja juu ya kufunga na kufungua pamoja nasi kwa vile mlikaa Uhispania masiku ya Ramadhaan[1].
Jibu: Hapana neno wala vibaya juu yenu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Fungeni kwa kuuona [mwezi] na fungueni kwa kuuona mwezi. Mkifunikwa na mawingu basi kamilisheni idadi ya [siku] thelathini.”[2]
Haya ni yenye kuenea kwa Ummah mzima. Saudi Arabia ndio nchi yenye haki zaidi kufuatwa kwa kujitahidi kwake kuhukumu kwa Shari´ah. Allaah azidi kuafikisha na kuiongoza. Isitoshe nyinyi mko katika nchi ambayo haihukumu kwa Uislamu na wala raia wake hawatilii umuhimu hukumu ya Uislamu.
Kuhusu swali lenu kuhusu kukusanya kati ya swalah mbili jambo lake ni lenye wasaa. Shari´ah safi imefahamisha juu ya kufaa kwake katika wakati wa mwanzo na wa pili au kati ya swalah mbili. Kwa sababu wakati wake umekuwa mmoja kwa haki ya yule ambaye amepewa udhuru kama kwa msafiri na mgonjwa. Vilevile inafaa kuzungumza kati ya swalah mbili zinazokusanywa kwa yale yanayopekea haja.
Kuhusu Witr wakati wake unaanza kuanzia pale mtu anapomaliza kuswali ´Ishaa ijapo ni yenye kukusanywa pamoja na Maghrib katika wakati wa swalah ya Maghrib.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/105-106).
[2] Muslim (1081) na an-Nasaa´iy (2124).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 64-65
Imechapishwa: 18/05/2022
https://firqatunnajia.com/47-kufuata-mwezi-mwandamo-wa-saudi-arabia-katika-nchi-isiyohukumu-kwa-shariah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)