Nabii ni yule ambaye Allaah anamfunulia Shari´ah na asimwamrishe kuifikisha. Mtume ni yule ambaye Allaah anamfunulia Shari´ah na pia akamwamrisha kuifikisha. Haya ndio maoni yaliyotangaa zaidi kuhusu tofauti kati ya Mtume na Nabii. Mtume ni yule ambaye ameamrishwa kufikisha. Maana yake ni kwamba ameamrishwa kuwalazimisha watu ujumbe na kupambana nao kwa ajili ya jambo hilo.

Vivyo hivyo Nabii anafunuliwa na anawalingania watu kwa Allaah (´Azza wa Jall), lakini anawafata Manabii wengine waliomtangulia, kupita juu ya njia yao na hapwekeki na Shari´ah yake maalum. Ni kama mfano wa Manabii wa wana wa israaiyl; walikuja na kulingania katika Tawraat ambayo Allaah aliiteremsha kwa Muusa (´alayhis-Salaam).

Mtunzi wa kitabu amesema:

“…na Mtume Wake aliyeridhiwa.”

Maana yake ni kwamba alikuwa ameteuliwa, amechaguliwa na ameridhiwa, kwa msemo mwingine Allaah amemridhia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 60
  • Imechapishwa: 06/12/2022