Aliyeteuliwa maana yake aliyechaguliwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ إِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ  وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ

“Wakumbuke waja Wetu – Ibraahiym na Ishaaq na Ya’quub – wenye nguvu na busara. Hakika Sisi tumewateua kutokana na Ikhlaasw zao kwa kuwapa sifa ya ukumbusho wa Aakhirah. Na hakika wao Kwetu bila shaka ni miongoni mwa walioteuliwa na walio bora kabisa.”[1]

Allaah (Subhaanah) alimchagua Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kati ya watu wake. Allaah ni mtambuzi zaidi ni wapi atakapoweka ujumbe Wake. Hamchagui isipokuwa yule ambaye anajua kuwa anastahiki kuchaguliwa na kwamba atasimamia kazi hiyo vilivyo. Kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na kubwa na kwa ajili hiyo Allaah hawachagui isipokuwa wale watu wenye kuiistahiki. Amesema (Subhaanah):

اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ

“Allaah anajua zaidi wapi aweke ujumbe Wake.”[2]

[1] 38:45-47

[2] 6:124

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 06/12/2022