Mbora na wa mwisho wa Mitume alikuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah yeye pia amemwita kuwa ni mja na akasema:

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

“Mkiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu, basi leteni Suurah mfano wake na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli.”[1]

Bi maana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile amesema (Ta´ala):

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”[2]

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Utakasifu ni wa Ambaye amemsafirisha mja Wake usiku kutoka al-Masjid al-Haraam mpaka al-Masjid al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake [amechukuliwa] ili Tumuonyeshe baadhi ya alama Zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima.”[3]

Mtu hawezi kuwa na nafasi ya juu na ya karibu zaidi kama kuwa mja wa Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msinisifu kwa kupindukia kama ambavyo manaswara walivyomsifu kwa kupindukia ´Iysaa mwana wa Maryam. Hakika mimi si venginevyo ni mja. Hivyo basi, semeni “Mja na Mtume wa Allaah”.”[4]

[1] 2:23

[2] 25:1

[3] 17:1

[4] al-Bukhaariy (3445).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 06/12/2022