46. Ni ipi hukumu ya kuswalia jeneza baada ya kuzikwa?

Swali 46: Ni ipi hukumu ya kuswalia jeneza baada ya kuzikwa? Je, kumewekwa kikomo cha mwezi[1]?

Jibu: Hukumu ya kuswalia jeneza baada ya kuzikwa ni Sunnah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswalia baada ya kuzikwa. Ambaye hakuhudhuria wakati wa kuswaliwa atamswalia baada ya kuzikwa. Hata yule ambaye amemswalia hapana vibaya kurudi kumswalia tena pamoja na waswaliji. Hapana neno kufanya hivo hata kama atamswalia mara mbili au mara tatu pamoja na wale wenye kumswalia miongoni mwa wale watu waliopitwa kumswalia. Kikomo kilichotangamaa kwa wanazuoni ni takriban mpaka mwezi mmoja.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/153).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 36
  • Imechapishwa: 23/12/2021