47. Maiti anaweza kuswaliwa baada ya kuzikwa kwa muda wa mwezi mmoja

Swali 47: Tumetambua kwamba kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba kumswalia maiti baada ya kuzikwa kunakuwa takriban mpaka mwezi mmoja. Vipi basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalia Maswahabah kule Baqiy´ mwishoni mwa uhai wake na kuwaombea du´aa[1]?

Jibu: Kilicholengwa kwa neno “kuswalia” ni kuwaombea du´aa. Ni ile du´aa anayoombewa maiti.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/154).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 37
  • Imechapishwa: 23/12/2021