Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ngazi ya kwanza: Uislamu una nguzo tano: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah… “

Kama alivosema mtunzi (Rahimahu Allaah) nguzo za Uislamu ni tano. Hizo ndio nguzo ambazo Uisamu umesimama juu yake. Hata hivyo zipo Shari´ah nyenginezo mbali na nguzo hizi tano. Kwa mfano kuwatendea wema wazazi wawili, kuwaunga ndugu, kutekeleza amana na mambo mengine ya lazima. Vivyo hivyo muislamu anatakiwa kujiepusha na mambo ya haramu mbali na nguzo hizi tano. Lakini hizi tano ndio nguzo ambazo hausimami isipokuwa kwazo.

1 – Shahaadah mbili: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kushuhudia ya kuwa Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nguzo hii ndio msingi wa

dini, msingi wa mila na ndio nguzo kubwa zaidi. Vilemiile ndio ufunguo wa Pepo. Muislamu anaingia ndani ya Uislamu kupitia shahaadah mbili na anakufa juu ya hizo mbili.

2 – Kusimamisha swalah: Amesema kusimamisha swalah na hakusema kuswali. Kusimamisha swalah ni kwa kule kuipa haki yake. Si kila mwenye kuswali anakuwa amesimamisha swalah. Wako wanaoswali lakini hawakuisimamisha. Waswaliji ni wengi na wenye kusimamisha swalah ni wachache. Kama ambavo wenye kuhiji ni wengi wanakaribia milioni tatu lakini hata hivyo ni wachache wanaotekeleza hajj kwa njia sahihi. Utaiona misikiti imejaa wenye kuswali. Lakini ni wangapi wenye kusimamisha swalah? Hivyo inakuwa kwa kuiswali kwa kumtakasia Allaah nia, kwa shauku na woga, kuitekeleza kwa sharti zake, mipaka yake, kusimama kunyooka, Rukuu´, kuuhudhurisha moyo ndani yake, kumfuata imamu, utulivu na kuiswali ndani ya wakati wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 71
  • Imechapishwa: 12/02/2023