46. Dalili ya kwamba kuna ambao walikuwa wakiwaabudu waja wema

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ

“Na Allaah atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili pasi naya Allaah?” Atasema: “Utakasifu ni Wako!” Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu.” (05:116)

MAELEZO

Mtajie maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

“Na Allaah atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!”

Mtajie haya ili ameze mawe ya kuwa kweli kuna makafiri waliokuwa wakiabudu mawalii na waja wema. Kwa hiyo hakuna tofauti kati yake na hawa makafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 63
  • Imechapishwa: 24/11/2023