45. Dalili ya kwamba kuna ambao walikuwa wakiwaabudu majini

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtajie maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ قَالُوا سُبْحَانَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم ۖ بَلْ كَانُوا يَعْبُدُونَ الْجِنَّ ۖ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ

“Na Siku Atakayowakusanya wote kisha atawaambia Malaika: “Je, hawa ndio waliokuwa wakikuabuduni?” Watasema: “Utakasifu ni Wako! Wewe ndiye bwana wetu sio hao!” Bali walikuwa wakiabudu majini, wengi wao wakiwaamini.” (34:40-41)

MAELEZO

Makusudio hapa ni kuwabainishia kuwa kuna makafiri waliokuwa wakiwaabudu Malaika, ambao ndio viumbe bora kabisa na mawalii wa Allaah. Hili linabatilisha utatizi wake ya kwamba tofauti kati yake na wao, ni kuwa anawaomba watu wema na mawalii, wakati wale wanawaomba masanamu, wafu na mfano wa hivyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 12/11/2023