Zakaah za nafaka, mifugo, thamani ya bidhaa na mavuno lazima zilipwe kwa mamlaka ya Kiislamu inayohusika na usambazaji. Haijuzu kwa yeyote kukataa kutoa zakaah au kujaribu kuepuka ulipaji wake kwa mamlaka. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu anayetaka kutoa zakaah:
“Tunaichukua na nusu ya mali yake.”[1]
Bi maana adhabu. Mamlaka itachukua zakaah na nusu ya mali yake. Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inafaa kwa mamlaka yoyote ya Kiislamu kuwaadhibu watu wasiotaka kulipa zakaah kwa njia ya kuchukua zakaah na nusu ya mali yake. Vivyo hivyo kuhusu aina nyenginezo za swadaqah za wajibu ambazo ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu; jukumu hilo itasimamia mamlaka ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zakaah ikitolewa kuipa mamlaka ya Kiislamu basi imetakasika dhimma ya mtu huyo. Dhimma imebaki kwa mamlaka. Ima wafanye uadilifu na hivyo walipwe thawabu, au wadhulumu na hivyo wastahiku kuadhibiwa. Hata hivyo haijuzu kukataa kumpa zakaah mtawala kwa sababu eti ni dhalimu. Bali ni wajibu kumpa nayo kwa ridhaa, nia njema na afikirie maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]
Vilevile Mtume mkarimu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninayokukatazeni jiepusheni nayo na ninayokuamrisheni yafanyeni kadri muwezavyo.”[3]
[1] Abu Daawuud (1575). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
[2] 64:16
[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 118-120
- Imechapishwa: 14/05/2026
Zakaah za nafaka, mifugo, thamani ya bidhaa na mavuno lazima zilipwe kwa mamlaka ya Kiislamu inayohusika na usambazaji. Haijuzu kwa yeyote kukataa kutoa zakaah au kujaribu kuepuka ulipaji wake kwa mamlaka. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu anayetaka kutoa zakaah:
“Tunaichukua na nusu ya mali yake.”[1]
Bi maana adhabu. Mamlaka itachukua zakaah na nusu ya mali yake. Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inafaa kwa mamlaka yoyote ya Kiislamu kuwaadhibu watu wasiotaka kulipa zakaah kwa njia ya kuchukua zakaah na nusu ya mali yake. Vivyo hivyo kuhusu aina nyenginezo za swadaqah za wajibu ambazo ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu; jukumu hilo itasimamia mamlaka ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zakaah ikitolewa kuipa mamlaka ya Kiislamu basi imetakasika dhimma ya mtu huyo. Dhimma imebaki kwa mamlaka. Ima wafanye uadilifu na hivyo walipwe thawabu, au wadhulumu na hivyo wastahiku kuadhibiwa. Hata hivyo haijuzu kukataa kumpa zakaah mtawala kwa sababu eti ni dhalimu. Bali ni wajibu kumpa nayo kwa ridhaa, nia njema na afikirie maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]
Vilevile Mtume mkarimu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninayokukatazeni jiepusheni nayo na ninayokuamrisheni yafanyeni kadri muwezavyo.”[3]
[1] Abu Daawuud (1575). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
[2] 64:16
[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 118-120
Imechapishwa: 14/05/2026
https://firqatunnajia.com/46-kuwapa-zakaah-mamlaka/