45. Safu zilizoko nje ya msikiti zinazotenganishwa na barabara

Swali 45: Kwa sababu ya msongamano mkubwa katika baadhi ya misikiti inayoswali ijumaa inatokea msikiti kujaa na hivyo baadhi ya watu wakaswali barabarani na njiani wakimfuata imamu. Unasemaje juu ya hilo? Je, kuna tofauti ikiwa njia iko kati ya waswaliji na msikiti?

Jibu: Ikiwa safu zimeungana hakuna neno. Vivyo hivyo hakuna neno ikiwa maamuma walioko nje ya msikiti wanaziona safu mbele yao au wanasikia Takbiyr ijapo ikiwa baadhi ya njia zimewatenganisha. Hilo ni kutokana na ulazima wa kuswali misikitini na wawe wanaweza kuwaona au kuwasikia. Lakini haifai kwa yeyote kuswali mbele ya imamu. Kwa sababu hiyo sio sehemu ya kusimama maamuma.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 30/08/2022