Miongoni mwa mambo yanayoenda kinyume na Shari´ah ni demokrasia na uchaguzi. Ni mambo ambayo hayana mafungamano yoyote na Shari´ah. Kwa mujibu wa ufahamu watu hawa wenyewe, inaenda kinyume na Shari´ah. Uchaguzi anashiriki ndani yake watenda madhambi, wanawake, manaswara, mayahudi, wakomunisti na kadhalika. Ni dhambi kushirikiana na watu hawa… hatuna mambo kama hayo.

Uchaguzi unaokubalika katika Shari´ah ni wakusanyike Ahl-ul-Hall wal-´Aqd, wakiwemo wanazuoni waliobobea na watu wa ´ibaadah na matendo mema, na wawachague wale wanawaona kuwa wanastahiki. Hivo ndivo alivyofanya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliteua watu wa mashauriano sita peke yao – watu sita hawa ndio ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa akiwa radhi nao. Hivyo wakamchagua ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Uchaguzi kama huu ndio unaokubalika katika Shari´ah na kikanuni, na si kila mtu kuzungumza ni nani ambaye anatakiwa kuwaongoza waislamu. Haijuzu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Aliy bin Aadam al-Ithyuubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=V16FubR1VWQ
  • Imechapishwa: 30/08/2022