Swali: Qunuut inasomwa namna gani katika Ramadhaan?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kusema:

اللهم اهدِنا فيمَن هديت وعافنا فيمن عافيت وتولنا فيمن توليت وبارك لنا فيما أعطيت وقِنا شر ما قضيت [ف]انك تقضي ولا يقضى عليك [و]اٍنه لا يذل مَن واليت [ولا يعزُ من عاديت]تباركت ربنا وتعاليت لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, nisalimishe pamoja na Uliowasalimisha na nilinde pamoja na Uliowalinda. Tubariki katika kile Ulichotupa na tukinge na shari ya Uliyotuhukumia. Kwani hakika Wewe unahukumu wala huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemlinda, na wala hatukuki Uliyemfanya adui[4]. Umebarikika, ee Mola wetu, na umetukuka. Hakuna mahali pa kuokoka kwengine isipokuwa Kwako.”[1]

[1] Ahmad (1727), Abu Daawuud (1425) na an-Nasaa’iy (1745). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Qiyaam Ramadhwaan, uk. 31-32”.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 37
  • Imechapishwa: 02/04/2022