Swali: Tunawaona watu wengi wanaswali katika Ramadhaan peke yake. Ramadhaan inapomalizika wanaihama misikiti. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huku ni kufahamu vibaya. Waislamu mnatakiwa kuhifadhi swalah katika Ramadhaan na miezi mingine. Ikiwa mmehifadhi swalah katika Ramadhaan na mkaona kuwa ni wajibu wa Uislamu, basi mnalazimika kuendelea juu ya jambo hilo. Hebu ifanyeni Ramadhaan iwe sababu ya kunyooka kwenu na kuendelea juu ya kheri. Ihifadhini kheri. Msiwe miongoni mwa wale wanaofanya matendo maovu baada ya kufanya matendo mazuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 38
  • Imechapishwa: 02/04/2022