44. Ni lini msafiri anatanguliza au anachelewesha?

Swali 44: Mtu akifika katika uwanja wa ndege wa Riyaadh baada ya swalah ya ´Ishaa ilihali hajaswali Maghrib na ´Ishaa – je, akusanye na afupishe Maghrib na ´Ishaa[1]?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa msafiri muda wa kuwa bado yuko safarini ni kufupisha. Kuhusu kukusanya ni jambo linahitaji upambanuzi. Akiwa bado yuko njiani anasafiri basi bora ni yeye kukusanya katika ule wakati wa swalah ya kwanza au katika ule wakati wa swalah ya pili kutegemea vile hali inavopelekea. Hayo ni kutokana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa anapokuwa bado yuko njiani basi anakusanya Maghrib na ´Ishaa na Dhuhr na ´Aswr. Ikiwa kuondoka kwake nyumbani ni kabla ya jua kupondoka, basi anacheleweshe Dhuhr na ´Aswr katika wakati wa swalah ya ´Aswr, na ikiwa kuondoka kwake ni baada ya jua kupondoka basi anatanguliza ´Aswr na Dhuhr na vivyo hivyo Maghrib na ´Ishaa. Ikiwa kuondoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya jua kuzama,  basi anachelewesha Maghrib na ´Ishaa katika wakati wa swalah ya ´Ishaa. Na ikiwa kuondoka kwake ni baada ya jua kuzama, basi anatanguliza ´Ishaa na Maghrib.

Bora kwa msafiri ni kutokusanya akiwa ameshatua. Kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hijjah ya kuaga hakukusanya kati ya swalah mbili katika hali ya kutua kwake Minaa.

Kuhusu ambaye ameshafika katika uwanja wa ndege wa Riyaadh ilihali hajaswali Maghrib na ´Ishaa, basi imesuniwa kwake kukusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa na aswali ´Ishaa kwa kufupisha. Kwa sababu katika wakati wa sasa uwanja wa ndege uko nje ya mji. Akichelewesha ´Ishaa na akaiswali kikamilifu pamoja na wengine ni sawa pia.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/285-286).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 15/05/2022