44. Namna ya kukamilisha swalah ya jeneza kwa aliyejiunga amechelewa

Swali 44: Mswaliji anatakiwa kulipa swalah ya jeneza akiingia akakuta amekwishapitwa na baadhi ya sehemu yake[1]?

Jibu: Atailipa papo hapo. Akijiunga na imamu katika Takbiyr ya tatu basi ataleta Takbiyr na kusoma al-Faatihah. Pindi imamu atapoleta Takbiyr ya nne basi naye ataleta Takbiyr ya pili kwa nisba yake na atamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati imamu atapoleta Tasliym basi naye ataleta Takbiyr ya tatu na atasema:

اللهم اغفر له وارحمه، وعافه واعف عنه، وأكرم نزله، ووسع مدخله واغسله بالماء والثلج والبرد، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس اللهم أبدله دارا خيرا من داره وأهلا خيرا من أهله، اللهم أدخله الجنة وأعذه من عذاب القبر ومن عذاب النار، وافسح له في قبره ونور له فيه، اللهم لا تحرمنا أجره ولا تضلنا بعده

“Ee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu. Ee Allaah! Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake na jamaa bora kuliko jamaa zake. Ee Allaah! Mwingize Peponi na mlinde kutokamana na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto. Mpanulie kaburi lake na muwekee nuru ndani yake. Ee Allaah! Usitunyime ujira wake na usitupoteze baada yake.”

Kisha atasema “Allaahu Akbar” mara ya nne na atatoa Tasliym.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/149-150).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 35
  • Imechapishwa: 22/12/2021