43. Mikono inanyanyuliwa sambamba na Takbiyr katika swalah ya jeneza

Swali 43: Je, ni Sunnah kunyanyua mikono sambamba na Takbiyr wakati wa kuswalia jeneza?

Jibu: Sunnah ni kunyanyua mikono sambamba na Takbiyr zote. Kutokana na yaliyothibiti kutoka kwa Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kuwa walikuwa wakiinyanyua sambamba na Takbiyr zote. Ameipokea ad-Daaraqutwniy kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Umar kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 20/12/2021