45. Kutangulizwe kumswalia maiti au swalah ya faradhi?

Swali 45: Mwenye kuingia msikitini kwa ajili ya kuswalia jeneza na bado hajaswali faradhi – je, aanze kuswali faradhi au ajiunge nao kuswalia jeneza? Jeneza likinyanyuliwa aliswalie[1]?

Jibu: Aswali pamoja nao kuliswalia jeneza kisha aswali faradhi. Kwa sababu jeneza linampita na faradhi haitomlipa. Jeneza likishanyanyuliwa asiliswalie. Atachofanya ni kulisindikiza na ataliswalia baada ya kuzikwa au kwenye kaburi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/151).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 22/12/2021