44. Msimamo wa Salaf uliosalimika juu ya watawala

Huu ndio msimamo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao sio kama Khawaarij na wafuasi wa Khawaarij katika kila zama na pahali ambao wanawafanyia uasi watawala kwa maneno mabaya. Maneno ya Khawaarij yanaziathiri nyoyo za raiai na hivyo wananza kuwachukia watawala, kuwatukana na kuwafanyia mikakati dhidi yao. Wanaendesha mitandano ya kisiri kwa ajili ya kuwang´oa watawala ambapo hali inakuwa mbaya. Kwa ajili hiyo ni sawa kabisa kukariri ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambayo inahusiana na kufanya subira, usaidizi, utiifu na usikizi. Wanakula viapo vya utiifu kwa watawala, mmoja baada ya mwengine. Atapokuja mwengine na kutaka kumpindua mtawala aliyepo hivi sasa watamshauri na kumtia khofu hata kama hatimaye itapelekea katika kumuua. Kwa hivyo ni nani mtawala huyu? Mtawala anaweza kuwa kwa moja kati ya njia zifuatazo:

1 – Anachaguliwa na wale wanaume wenye ufahamu na wanazuoni.

2 – Anayeteuliwa na yule mtawala aliyetangulia na akaridhiwa na wale watu wenye busara.

3 – Akampindua yule mtawala aliyepo hivi sasa na hali ikatulia chini ya udhibiti wake. Endapo yule mpanga mapinduzi atamg´oa mtawala aliyepo hivi sasa na raia wasiweze kukabiliana na mtawala huyo dhalimu mpaka akafanikiwa kuituliza hali chini ya udhibiti wake, basi itatakiwa kwa raia kumsikiliza na kumtii mtawala huyu mpya aliyeshinda kwa mabavu yake. Baada ya hapo haitojuzu kumfanyia uasi kwa sababu eti kamdhulumu yule mtawala wa kwanza. Huyu wa pili pia anatakiwa kusikilizwa na kutiiwa katika mema na kuzingatiwa kuwa ni mtawala kwa mujibu wa Shari´ah.

Hii ndio misimamo ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, Salaf na wafuasi wao wakapita juu ya nyayo zao hadi hii leo. Kwa hivyo hawafanyi kama Khawaarij wala kama Raafidhwah. ´Aqiydah yao imesalimika na mfumo wao ni sahihi, ambayo inatokana na dalili za wazi kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah kwa mujibu wa ufahamu wa Salaf. Allaah awawie radhi na kuwarehemu na kuwalipa mabustani ya Pepo.

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 14/05/2026