Jeshi la Allaah ndio washindi kwa hoja na kwa ulimi, kama ambavyo wanashinda kwa panga na kwa mikuki.

MAELEZO

Amesema (Ta´ala):

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ

”Hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda.” (37:173)

Amelinasibisha jeshi Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Jeshi la Allaah ni waumini. Wao ndio huitwa ´jeshi la Allaah` na pia huitwa ´kundi la Allaah`. Amesema (Ta´ala):

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ

“Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho wanafanya urafiki na kuwapenda ambaye anapinzana na Allaah na Mtume Wake.” (58:22)

أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.” (58:22)

Wao ni kundi na jeshi la Allaah. Jeshi ni wingi wa mwanajeshi – جندي – naye ni yule mpambanaji na anayeitetea dini ya Allaah. Amewaegemeza Kwake kwa ajili ya kuwatukuza. Vilevile amewafanya ni wenye kushinda kwa hoja na silaha.

Jeshi la Allaah ndio washindi… – Bi maana kwa elimu, maarifa na kuwajadili watu wa batili. Kamwe watu wa batili hawakabiliani na Ahl-ul-Haqq isipokuwa Ahl-ul-Haqq huwashinda daima katika magomvi na mijadala. Wao huwashinda watu wa batili kwa hoja kama ambavyo hushinda uwanjani kwa silaha na mikuki. Jeshi la waislamu likikutana na makafiri basi waislamu huwashinda makafiri endapo watatimiza masharti ya nusura. Hapa ni pale watapomtegemea Allaah, wakashikamana Naye, wakamtii Yeye na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kukitokea kasoro kati yao basi wanashindwa kama ilivyowatokea baadhi ya Maswahabah wakati wake pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaamrisha wasishuke kutoka mlimani ambao alikuwa amewaambia:

“Msishuke kutoka mlimani sawa tukishinda au tukishindwa.”

Walipoenda kinyume na wakashuka kutoka mlimani ndipo wakashindwa[1].

[1] al-Bukhaariy (48/26).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 61
  • Imechapishwa: 16/12/2016