44. Ambaye amechelewa kile anachowahi katika swalah ndio mwanzo au mwisho wa swalah yake?

Swali 44: Je, zile Rak´ah ambazo anawahi nyuma ya imamu yule ambaye amekuja amechelewa inazingatiwa ndio mwanzoni mwa swalah yake au mwishoni mwake? Kama kwa mfano amekosa Rak´ah mbili katika swalah ya Rak´ah nne imesuniwa kwake kusoma kile kitachomuwepesikia baada ya al-Faatihah?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba yale anayowahi ambaye amekuja amechelewa nyuma ya imamu yanazingatiwa ndio sehemu ya mwanzo ya swalah yake na yale anayolipa ndio sehemu ya mwisho katika swalah zote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Itapokimiwa swalah basi tembeeni na lazimianeni na utulivu. Kile mtachowahi kiswalini na kile kitachokupiteni kikamilisheni.”

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Kwa ajili hiyo inapendeza kufupika na kisomo cha al-Faatihah katika ile Rak´ah ya tatu, kama vile Maghrib, na ile Rak´ah ya nne. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma katika Dhuhr na ´Aswr katika zile Rak´ah mbili za mwanzo ufunguzi wa Kitabu na Suurah nyingine ambapo anarefusha katika ile Rak´ah ya kwanza na anafupisha katika ile Rak´ah ya pili na Rak´ah mbili za mwisho anasoma ufunguzi wa Kitabu.”

Ni vizuri ikiwa baadhi ya wakati atasoma zaidi ya al-Faatihah katika Rak´ah ya tatu na Rak´ah ya nne kukiwemo swalah ya Dhuhr. Hilo ni kutokana na yale yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma katika [Rak´ah] mbili za mwanzo kiwango cha Alif Laam Miym Tanziyl as-Sajdah, katika [Rak´ah] mbili za mwisho nusu yake, katika [Rak´ah] mbili za mwanzo za ´Aswr kwa kiwango cha zile za mwisho za Dhuhr na katika [Rak´ah] mbili za mwisho za ´Aswr kwa kiwango cha nusu yake.”

Haya yanafasiriwa kwa njia ya kwamba alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya hivo baadhi ya nyakati katika Rak´ah mbili za mwisho za Dhuhr kwa ajili ya kuoanisha kati ya Hadiyth mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 30/08/2022