44. Allaah ndiye ninayemwabudu na sina mwabudiwa mwengine zaidi Yake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yeye ndiye ninayemwabudu na sina mwabudiwa mwingine asiyekuwa Yeye.” 

MAELEZO

Yeye ndiye ninayemwabudu – Mola ambaye hii ndio shani yake Yeye ndiye ambaye mimi na wengine wanastahiki kumwabudu. Jengine ni kwamba Shaykh (Rahimahu Allaah) ameweka wazi kuwa haitoshi kukubali uola. Haitoshi wewe kusema kuwa Mola wako ni Allaah ambaye amekulea kwa neema Zake. Haya hayatoshi. Ni lazima vilevile kumkubalia ´ibaadah na kumtakasia Yeye ´ibaadah. Hii ndio tofauti kati ya mpwekeshaji na mshirikina. Mpwekeshaji anakubali uola wa Allaah (´Azza wa Jall) na kumfanyia ´ibaadah pekee hali ya kuwa hana mshirika. Mshirikina anakubali uola wa Allaah pamoja na kwamba anashirikisha katika ´ibaadah Yake. Anashirikisha pamoja na wengine katika ´ibaadah Yake. Anashirikisha pamoja Naye wale ambao hawaumbi, hawaruzuku na wala hawamiliki chochote. Hii ndio tofauti kati ya mpwekeshaji na mshirikina. Mpwekeshaji anasema kuwa Mola Wake ni Allaah, ndiye anayemwabudu na kwamba hana mwabudiwa mwengine asiyekuwa Yeye. Ama mshirikina anasema kuwa Mola Wake ni Allaah lakini hamwabudu Allaah peke yake. Hivyo anaabudu miti, mawe, mawalii, waja wema na makaburi pamoja na Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana ikawa mshirikina na kukubali kwake uola wa Allaah hakukumfaa chochote na wala hakukumfanya kuingia ndani ya Uislamu.

Ndiye ninayemwabudu – Bi maana Mungu ninayemwabudu.

Sina mwabudiwa mwengine asiyekuwa Yeye – Si katika Malaika, Mitume, waja wema, miti, mawe wala chochote kile. Sina mwabudiwa mwengine asiyekuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Huku ni kuithibitisha Tawhiyd kwa dalili. Hii ni dalili ya kiakili. Kisha akataja dalili ya kinukuu kutoka katika Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 15/12/2020