43. Radd ya kwanza juu ya makafiri wenye kupinga kufufuliwa

Miongoni mwa shubuha zao ni kuwa wanasema kuwa viwiliwili hivyo vimeshakuwa udongo na kusagika na kuoza?

أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ

”Je, hata tukiwa ni mifupa iliyosagika na kuoza? Watasema: ”Basi marejeo hayo ni yenye khasara.”[1]

Ni vipi vitarudi kuwa na uhai baada ya kuoza na kuwa mifupamifupa?

وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا

“Wakasema: “Je, hivi sisi tukiwa mifupa na mapande yaliyosagikasagika hivi sisi hivyo tutafufuliwa katika umbo jipya?”[2]

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌٌ

“Akatupigia mfano akasahau kuumbwa kwake; akasema: “Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshasagika na kuwa kama vumbi.”[3]

Wanaona kuwa ni jambo haliwezekani kabisa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewaraddi kwa Ruduud mbalimbali kukiwemo:

Yule ambaye alianzisha uumbaji wao ana haki zaidi ya kuweza kuwarudisha. Yule ambaye ana uwezo wa kuanzisha ana haki zaidi ya kuweza kuwarudisha:

وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

”Naye ndiye aliyeanzisha uumbaji, kisha anaurudisha, nayo ni mepesi mno Kwake – Naye ana wasifu wa juu kabisa katika mbingu na ardhi.”[4]

Allaah (´Azza wa Jall) kila jambo Kwake ni jepesi. Lakini hili ni kwa njia ya kupiga mfano uingie akilini. Akili ina

jua kuwa kulirudi jambo ni kwepesi kuliko kulianzisha. Mtu akija na akaunda chombo kwa misumari na vitu vinavyohitajia umakini mkubwa. Kisha baada ya hapo chombo hichi kikaharibika na kusambukasambuka kila kipande sehemu yake – je, yule aliyekiunda mara ya kwanza si ni muweza wa kukiunda kwa wepesi zaidi mara ya pili? Jibu ni ndio. Kwa sababu ameshakijua na anajua mahali pa kila kifaa na kila msumari. Mhanhidi ambaye amekitengeneza mara ya kwanza ni rahisi kwake kurudi kukitengeneza upya. Hapa ni kwa njia ya kutumia akili. Ambaye amekianza kitu ana haki zaidi ya kuweza kukirudi. Kwa ajili hiyo amesema:

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ

“Akatupigia mfano akasahau kuumbwa kwake… ”

Amesahau kuwa Allaah ndiye amemuumba kutoka katika kutokuweko:

قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ

”Akasema: “Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshasagika na kuwa kama vumbi.” Sema: “Ataihuisha Yule aliyeianzisha mara ya kwanza Naye ni mjuzi wa kila [namna ya] kuumba.””[5]

Ambaye ameweza kukianza kitu ana haki zaidi ya kuweza kukirudi. Hili ni kwa mtazamo wa akili. Vinginevyo Allaah (Jalla wa ´Alaa) hashindwi na kitu. Hayo ni kwa njia ya kutaka kuwafahamisha watu hawa.

[1] 79:11-12

[2] 17:49

[3] 36:78

[4] 30:27

[5] 36:78-79

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 06/04/2021