43. Baadhi ya hukumu zinazomuhumu mwanamke katika Hajj na ´Umrah IX

7 – Inajuzu kwa mwanamke katika hali ya Ihraam yake kuvaa nguo za wanawake anazotaka zisizokuwa na mapambo, hazifanani na nguo za wanaume, si zenye kubana kuonyesha fomu ya viungo vyake, si nyepesi zenye kuonyesha kilicho nyuma yake na si fupi zenye kuishilia kwenye miguu yake au mikononi mwake. Bali nguo hizo zinatakiwa kuwa pana na nene. Ibn-ul-Mundhir amesema:

“Wanachuoni wameafikiana kuwa inafaa kwa mwanamke mwenye kuhirimia kuvaa kanzu, Duruu´, shuka ya chini na soksi za ngozi.”[1]

Si lazima kwake kuvaa nguo yenye rangi maalum kwa mfano nyekundu. Bali anachotakiwa ni yeye kuvaa anachotaka katika rangi ambazo ni maalum kwa wanawake kama nyekundu, kijani kibichi au nyeusi. Akitaka inafaa kwake kuibadilisha kwa nguo nyingine.

8 – Imesuniwa kwake kuleta Talbiyah baada ya Ihraam kwa kiasi cha vile atavyojisikia mwenyewe. Ibn-ul-Mundhir amesema:

“Wanachuoni wameafikiana kwamba Sunnah kwa mwanamke ni yeye asinyanyua sauti yake. Anachotakiwa ni yeye kuisikilizisha nafsi yake mwenyewe. Imechukizwa kwake kunyanyua sauti yake kwa kuchelea kufitinika kwake. Kwa ajili hiyo si Sunnah kwake kuleta adhaana wala Iqaamah. Kilichopendekezwa kwake wakati wa kutaka kuzindua jambo katika swalah ni kupiga makofi na si kusema “Subhaan Allaah”.[2]

[1] al-Mughniy (03/328).

[2] al-Mughniy (03/330-331).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 13/11/2019