Swali 42: Mtu ambaye anaenda kinyume na kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa katika suala la kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah au katika suala la kuwasikiliza na kuwatii watawala, mwema na muovu wao, muda wa kuwa hawajaamrisha maasi anatoka nje hata kama anaafikiana nao katika mambo mengine ya ´Aqiydah?
Jibu: Ndio. Akienda kinyume nao katika jambo fulani na akaafikiana nao katika jambo lingine, basi hawi katika wao katika yale ambayo ameenda kinyume nao na yuko katika wao katika yale ambayo ameenda sambamba nao. Mtu kama huyo yumo katika khatari kubwa na anaingia ndani ya makemeo:
” Na ummah wangu utagawanyika katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
Anaweza kuingia Motoni kwa sababu ya kwenda huku kinyume. Haijalishi kitu hata kama ni kwenda kinyume na katika jambo moja tu la ´Aqiydah. Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
hayana maana kuwa wote ni makafiri naa watadumishwa Motoni milele. Wataingia Motoni kwa kiasi cha kwenda kwao kinyume. Wakati fulani pengine kwenda kinyume kukamtoa mtu nje ya dini na pengine wakati mwingine kusimtoe mtu nje ya dini.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 128-129
- Imechapishwa: 27/02/2024
- Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Swali 42: Mtu ambaye anaenda kinyume na kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa katika suala la kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah au katika suala la kuwasikiliza na kuwatii watawala, mwema na muovu wao, muda wa kuwa hawajaamrisha maasi anatoka nje hata kama anaafikiana nao katika mambo mengine ya ´Aqiydah?
Jibu: Ndio. Akienda kinyume nao katika jambo fulani na akaafikiana nao katika jambo lingine, basi hawi katika wao katika yale ambayo ameenda kinyume nao na yuko katika wao katika yale ambayo ameenda sambamba nao. Mtu kama huyo yumo katika khatari kubwa na anaingia ndani ya makemeo:
” Na ummah wangu utagawanyika katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
Anaweza kuingia Motoni kwa sababu ya kwenda huku kinyume. Haijalishi kitu hata kama ni kwenda kinyume na katika jambo moja tu la ´Aqiydah. Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
hayana maana kuwa wote ni makafiri naa watadumishwa Motoni milele. Wataingia Motoni kwa kiasi cha kwenda kwao kinyume. Wakati fulani pengine kwenda kinyume kukamtoa mtu nje ya dini na pengine wakati mwingine kusimtoe mtu nje ya dini.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 128-129
Imechapishwa: 27/02/2024
Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/42-mtu-ambaye-anatofautiana-na-ahl-us-sunnah-katika-jambo-moja-tu-la-aqiydah-anatoka-nje/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket