Swali 41: Wako wanaotofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka? Je, ni sahihi kufarikisha? Mambo yakishakuwa hivo ni kina nani hao kundi lililookoka? Ni kina nani hao kundi lililonusuriwa?
Jibu: Hawa wanataka kufarikisha kila kitu. Wanataka kutenganisha kati ya waislamu. Mpaka sifa za waislamu wanataka kutenganisha kati yazo. Maneno haya si sahihi. Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka[1]. Haliwi lenye kunusuriwa mpaka liwe limeokoka na wala haliwi lenye kuokoka mpaka liwe lenye kunusuriwa. Ni sifa mbili zinazolazimiana juu ya kitu kimoja. Kutenganishwi huku ima kunafanywa na mjinga au mtu mwenye malengo mabaya ambaye anataka kuwatia mashaka vijana waislamu juu ya kundi kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka[2].
[1] Haya ndio maoni ya maimamu wa Ahl-ul-Hadiyth. Kundi lililookoka ndio kundi lililonusuriwa na ndio Ahl-ul-Hadiyth, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, al-Jamaa´ah na Salafiyyuun. Hayo yamesemwa wazi na kikosi kikubwa cha Salaf na wale waliokuja nyuma. Hii hapa baadhi ya mifano:
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema kwa mnasaba wa Hadiyth ”Na Ummah wangu utagawanyika… ”
”Ikiwa sio Ahl-ul-Hadiyth basi sitambui ni kina nani.”
Ameipokea al-Haakim katika ”Ma´rifatu ´Uluum-il-Hadiyth”, uk. 3, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
al-Mubaarakfuuriy ametaja mwanzoni mwa ”Tuhfat-ul-Ahwadhiy” kwamba Abul-Yumn bin ´Asaakir amesema:
”Hebu Ahl-ul-Hadiyth wafurahi na bishara njema hii… Wao – Allaah akitaka – ndio kundi lililookoka.” (Uk. 13)
at-Tirmdhiy amesema wakati wa Hadiyth ”Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu… ”
”Nimemsikia al-Bukhaariy akisema kuwa amemsikia Ibn-ul-Madiyniy akisema: ”Wao ni Ahl-ul-Hadiyth.”” (2229)
al-Bukhaariy amesema katika ”Khalq Af´aal-il-´Ibaad” punde tu baada ya Hadiyth ya Abu Sa´iyd kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):
كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا
“Ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah kati na kati na adilifu.” (21:143)
”Hao ni lile kundi lililotajwa katika Hadiyth ”Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu… ”.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah hakutofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka. Bali mwanzoni mwa ”al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” amesema:
”Hii ni ´Aqiydah ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, mpaka kisimame Qiyaamah.”
Vivyo hivyo ndivo alivofanya katika ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (3/129).
Amesema tena:
”Maoni yangu ni ile ´Aqiydah ya kundi lililookoka. Nalo ni lile kundi lililoosifiwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuokoka. Hiyo ndio ´Aqiydah iliyosimuliwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum). Wao na wale wenye kuwafuata ndio kundi lililookoka.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (3/179))
[2] Kuna mtu ambaye anajinasibisha na elimu amejichosha, akapoteza wakati wake na akawachanganya vijana wakati alipoandika kitabu ambapo anataka kuthibitisha kuwa kuna tofauti kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka. Hakufanikiwa na wala katu hatofanya hivo. Alifanya hali kuwa mbaya zaidi pale alipomzulia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na akadai kuwa anayatofautisha, pasi na marejeo yoyote. Hayo amaeyaandika katika kitabu kwa jina ”al-Ghurabaa’ al-Awwaluun”. Kisha akaenda mbali zaidi na kudai kuwa hata Imaam ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ana maoni hayo. Wakati alipoulizwa katika muhadhara juu ya tofauti ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka akasema:
”Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ameafikiana na mimi juu ya hilo. Ameniahidi kuandika maelezo yaliyo na jambo hilo.”
Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amemfichukua kwa vile Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz haafikiani naye kabisa wakati alipoulizwa juu ya hilo. Hapa chini yanakuja maswali na jawabu lake:
Swali: Je, ni kweli kuwa unatofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka?
Jibu: Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka. Ni moja.
Swali: Huyatofautishi kati yake?
Jibu: Ni moja.
Swali: X jana jioni alikuwa na muhadhara na akasema kuwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz anaafikiana naye juu ya hilo.
Jibu: Hapana, hapana. Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao ni Ahl-us-Sunnah, kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa.
Swali: Na wao ni Salafiyyuun?
Jibu: Na wao ni Salafiyyuun. Wao ni kundi lililookoka kwa sababu wameokoka kutokana na Moto, wao ni kundi lililonusuriwa kwa sababu wameahidiwa kunusuriwa na wao ni Ahl-us-Sunnah kwa sababu wanazifuata Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). (https://www.youtube.com/watch?v=9jJcabonJGM&app=desktop)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 126-128
- Imechapishwa: 27/02/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Swali 41: Wako wanaotofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka? Je, ni sahihi kufarikisha? Mambo yakishakuwa hivo ni kina nani hao kundi lililookoka? Ni kina nani hao kundi lililonusuriwa?
Jibu: Hawa wanataka kufarikisha kila kitu. Wanataka kutenganisha kati ya waislamu. Mpaka sifa za waislamu wanataka kutenganisha kati yazo. Maneno haya si sahihi. Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka[1]. Haliwi lenye kunusuriwa mpaka liwe limeokoka na wala haliwi lenye kuokoka mpaka liwe lenye kunusuriwa. Ni sifa mbili zinazolazimiana juu ya kitu kimoja. Kutenganishwi huku ima kunafanywa na mjinga au mtu mwenye malengo mabaya ambaye anataka kuwatia mashaka vijana waislamu juu ya kundi kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka[2].
[1] Haya ndio maoni ya maimamu wa Ahl-ul-Hadiyth. Kundi lililookoka ndio kundi lililonusuriwa na ndio Ahl-ul-Hadiyth, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, al-Jamaa´ah na Salafiyyuun. Hayo yamesemwa wazi na kikosi kikubwa cha Salaf na wale waliokuja nyuma. Hii hapa baadhi ya mifano:
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema kwa mnasaba wa Hadiyth ”Na Ummah wangu utagawanyika… ”
”Ikiwa sio Ahl-ul-Hadiyth basi sitambui ni kina nani.”
Ameipokea al-Haakim katika ”Ma´rifatu ´Uluum-il-Hadiyth”, uk. 3, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
al-Mubaarakfuuriy ametaja mwanzoni mwa ”Tuhfat-ul-Ahwadhiy” kwamba Abul-Yumn bin ´Asaakir amesema:
”Hebu Ahl-ul-Hadiyth wafurahi na bishara njema hii… Wao – Allaah akitaka – ndio kundi lililookoka.” (Uk. 13)
at-Tirmdhiy amesema wakati wa Hadiyth ”Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu… ”
”Nimemsikia al-Bukhaariy akisema kuwa amemsikia Ibn-ul-Madiyniy akisema: ”Wao ni Ahl-ul-Hadiyth.”” (2229)
al-Bukhaariy amesema katika ”Khalq Af´aal-il-´Ibaad” punde tu baada ya Hadiyth ya Abu Sa´iyd kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):
كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا
“Ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah kati na kati na adilifu.” (21:143)
”Hao ni lile kundi lililotajwa katika Hadiyth ”Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu… ”.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah hakutofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka. Bali mwanzoni mwa ”al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” amesema:
”Hii ni ´Aqiydah ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, mpaka kisimame Qiyaamah.”
Vivyo hivyo ndivo alivofanya katika ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (3/129).
Amesema tena:
”Maoni yangu ni ile ´Aqiydah ya kundi lililookoka. Nalo ni lile kundi lililoosifiwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuokoka. Hiyo ndio ´Aqiydah iliyosimuliwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum). Wao na wale wenye kuwafuata ndio kundi lililookoka.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (3/179))
[2] Kuna mtu ambaye anajinasibisha na elimu amejichosha, akapoteza wakati wake na akawachanganya vijana wakati alipoandika kitabu ambapo anataka kuthibitisha kuwa kuna tofauti kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka. Hakufanikiwa na wala katu hatofanya hivo. Alifanya hali kuwa mbaya zaidi pale alipomzulia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na akadai kuwa anayatofautisha, pasi na marejeo yoyote. Hayo amaeyaandika katika kitabu kwa jina ”al-Ghurabaa’ al-Awwaluun”. Kisha akaenda mbali zaidi na kudai kuwa hata Imaam ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ana maoni hayo. Wakati alipoulizwa katika muhadhara juu ya tofauti ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka akasema:
”Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ameafikiana na mimi juu ya hilo. Ameniahidi kuandika maelezo yaliyo na jambo hilo.”
Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amemfichukua kwa vile Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz haafikiani naye kabisa wakati alipoulizwa juu ya hilo. Hapa chini yanakuja maswali na jawabu lake:
Swali: Je, ni kweli kuwa unatofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka?
Jibu: Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka. Ni moja.
Swali: Huyatofautishi kati yake?
Jibu: Ni moja.
Swali: X jana jioni alikuwa na muhadhara na akasema kuwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz anaafikiana naye juu ya hilo.
Jibu: Hapana, hapana. Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao ni Ahl-us-Sunnah, kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa.
Swali: Na wao ni Salafiyyuun?
Jibu: Na wao ni Salafiyyuun. Wao ni kundi lililookoka kwa sababu wameokoka kutokana na Moto, wao ni kundi lililonusuriwa kwa sababu wameahidiwa kunusuriwa na wao ni Ahl-us-Sunnah kwa sababu wanazifuata Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ()
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 126-128
Imechapishwa: 27/02/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/41-je-ni-sahihi-kutofautisha-kati-ya-kundi-lililonusuriwa-na-kundi-lililookoka/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)