Swali: 40: Je, ulinganizi wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ni ulinganizi wa Kiislamu wa kivyamavyama kama vile ulinganizi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun na ulinganizi wa Jamaa´at-ut-Tabliygh? Unamnasihi nini anayesema maneno haya na kuyaeneza ndani ya vitabu?
Jibu: Ulinganizi wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ni wenye kuafikiana na mfumo wa Salaf inapokuja katika misingi na tanzu[1]. Malengo yake sio kufupika na kundi fulani kinyume na yale waliyokuwemo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika zama zote.
Kuhusu makundi kama vile al-Ikhwaaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliygh na mengineyo[2], sisi tunawaita wote wairudishe mifumo yao katika Qur-aan, Sunnah na mwongozo na ufahamu wa Salaf na wayapime na hayo. Kile kinachoafikiana navyo, ni vyema na himdi zote anastahiki Allaah, na kile kinachoenda kinyume navyo basi kosa linatakiwa kurekebishwa. Haya ndio ambayo tunalingania kwayo.
[1] Vitabu vyake (Rahimahu Allaah) vipo. Vinabainisha ´Aqiydah sahihi, Tawhiyd (ambayo ndio haki ya Allaah kwa waja) na kubainisha yanayopingana nayo. Aliwalingania watu kumwabudu Allaah pekee na kutupilia mbali mengine yote. Huo ndio ulinganizi wa Mitume wote (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Huo ndio ulinganizi wa imamu mwenye kufanya upya ambaye kwa ulinganizi wake Allaah ameihuisha miji na watu. Mpaka hii leo bado tunaendelea kuishi chini ya kivuli cha ulinganizi wake uliobarikiwa – na himdi zote njema ni stahiki ya Allaah.
[2] Je, mwanzilishi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun au mmoja katika wafuasi wake mpaka hii leo ameandika kitabu kimoja tu kuhusu Tawhiyd na akibainisha ´Aqiydah sahihi? Je, Hasan al-Bannaa alilingania kuhus kumtakasia ´ibaadah Allaah (Ta´ala) na kuitupilia mbali shirki kwa sampuli zake zote? Je, ameyatokomeza makuba? Je, ameyasawazisha makaburi? Je, amekataza kufanya Tawassul kwenye makaburi ya wale wanaowaita waja wema na mawalii? Je, amesimamisha Sunnah? Maswali yote haya hayana majibu ya uthibitisho. Jibu analo ambaye anaijua ´Aqiydah ya Salaf, akailinganisha na ulinganizi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun inayowakilishwa na mwanzilishi wake Hasan al-Bannaa na akavisoma vitabu vyake. Ataona kuwa al-Bannaa hakuwa na ulinganizi wa wazi na wa dhati katika kupambana na shirki na Bid´ah. Mambo ni kinyume. Hasan al-Bannaa amesema:
”Nilikuwa pamoja na ndugu Hasswaafiyyah Damanhur. Kila usiku nilihudhuria katika msikiti Tawbah.” (Mudhakkiraat-ud-Da´wah wad-Daa´iyah, uk. 24)
Je, huu ni ulinganizi wa kuisafisha ´Aqiydah? Amesema katika kitabu hichohicho:
”Alihudhuria as-Sayyid ´Abdul-Wahhaab (ambaye anajuzisha mrengo wa Hasswaafiyyah). Nilichukua Hasswaafiyyah Shaadhiliyyah kutoka kwake. Aliniidhinisha kusomesha nyuradi na kazi zake.” (Uk. 24)
Amesema tena:
”Masiku ya Damanhur yalikuwa yamejaa shauku ya Taswawwuf. Ilikuwa ni kipindi kilichojaa ´ibaadah na Taswawwuf.” (Uk. 28)
Amesema pia:
”Masiku mengi ya ijumaa tulikuwa tukiyatumia Damanhur. Tulikuwa tukimtembelea mmoja katika mawalii na waja wa waliokurubishwa Damanhur. Wakati mwingine tukitembelea Dasuuq. Tukitembea kwa miguu punde tu baada ya Fajr na kufika takriban saa mbili asubuhi. Tukitembea kwa masaa matatu. Kulikuwa na umbali wa takriban 20 km. Tukitembelea kaburi, tukiswali swalah ya ijumaa na tukipumzika. Baada ya hapo tunarudi Damanhur.” (Uk. 30)
Hakusikia maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:
”Msifunge safari isipokuwa kuiendea misikiti mitatu… ”? (al-Bukhaariy (1132) na Muslim (1397))
Hasan al-Bannaa amesema:
”Wakati fulani tulikuwa tukimtembelea ´Uzbah an-Nawwaam kwa sababu katika makaburi hayohayo alikuwa amezikwa Shaykh Sayyid Sinjar, mmoja katika wanamme vigogo wa mrengo wa Hasswaafiyyah ambaye alikuwa anatambulika kwa wema na uchaji wake. Tukibaki huko siku nzima kisha baadaye tukirudi.” (Uk. 30)
Amesema tena:
”Nakumbuka ya kwamba katika desturi yetu tulikuwa tukifanya gwaride kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tulikuwa tukifanya hivo kila jioni baada ya ´uhudhuriaji`, kuanzia mwanzo wa Rabiy´ al-Awwaal mpaka tarehe kumi na mbili Rabiy´ al-Awwaal. Tukifanya gwaride na tukiimbia mashairi yaliyozoeleka kwa furaha kamili.” (Uk. 52)
Miongoni mwa mashairi ilikuwa ni:
Mpenzi huyu pamoja na wapenzi amehudhuria
na amemsamehe kila mmoja kwa madhambi yale yaliyotangulia
Amesema tena:
”Kutafuta ukaribu wa Allaah kupitia mmoja katika viumbe, Tawassul, ni tofauti ya tanzu inayohusiana na namna ya kufanya du´aa. Sio katika mambo yanayohusu ´Aqiydah.” (Majmuu´ Rasaa-il Hasan al-Banna, uk. 392)
Haya hayahitaji maelezo. Bwana huyu alikuwa Suufiy, Hasswaafiy na mwabudia makaburi. Amempa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sifa ya Muumbaji pinid aliposema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasamehe. Hakumbakizia Allaah chochote. Allaah ametakasika kutokana na wanayoyasema. Amesema vilevile wakati alipokuwa anazumgumzia majina na sifa za Allaah:
”Vovyote mtu atakavyozungumzia jambo hili linapelekea katika natija moja, nayo ni kwamba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ndiye anayejua nini maana yake.” (Majmuu´ Rasaa-il Hasan al-Banna, uk. 452)
Nimepata maneno ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) akiwazungumzia Mufawwidhwah ambao wanasema kuwa Allaah pekee ndiye anayejua maana ya sifa Zake na kwamba wao ndio Ahl-ul-Bid´ah waovu kabisa. Amesema:
”Kuhusu Tafwiydhw, ni jambo lenye kutambulika kuwa Allaah (Ta´ala) ametuamrisha kuizingatia Qur-aan na akatuhimiza kuielewa na kuifahamu. Ni vipi pamoja na hayo itawezekana tutakiwe kutoitambua, kutoijua na kuielewa… Hayo yakafahamisha kuwa Mufawwidhwah, ambao wanadai wanafuata Sunnah na Salaf, ni miongoni mwa aina mbaya kabisa za Ahl-ul-Bid´ah na wapotofu.” (Dar’ Ta´aarudhw-il-´Aql wan-Naql (6/201-205)
Je, inawezakana kwa mtu ambaye ana upeo mdogo kabisa wa elimu na akili kufanya ulinganisho japo mdogo kabisa kati ya ulinganizi wa Imaam na Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na ulinganizi uliokuwa ukifanywa na muhuishaji wao wa Bid´ah? Tofauti ni kubwa kabisa kati ya nyota na udongo.
Imaam na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun. Hapa chini kuna swalli lenyewe na jawabu:
Swali: al-Ikhwaan al-Muslimuun wameingia Saudi Arabia tangu kipindi fulani. Wamekuwa ni wenye uchangamfu kati ya wanafunzi. Unasemaje juu ya harakati hizi na ni kiasi gani imeafikiana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
Jibu: al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekosolewa na wanazuoni wakubwa kwa kuwa hawatilii umuhimu kulingania katika Tawhiyd na kukemea shirki na Bid´ah. Wana njia maalum ambazo nafasi zake zinafanya kutolingania kwa Allaah na ´Aqiydah sahihi walionayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. al-Ikhwaan al-Muslimuun wanatakiwa kutilia umuhimu wa kulingania kwa mujibu wa ulinganizi wa Salafiyyah na kulingania kwa Allaah na kukataza kuyaabudia makaburi, kuwategemea wafu, kuwataka msaada wafu kama al-Husayan, al-Badawiy au wengine. Wanatakiwa kutilia umuhimu msingi huu mkuu, nayo ni maana ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` ambayo ndio msingi wa dini. Kitu cha kwanza ambacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalingania wakazi wa Makkah ni kumpwekesha Allaah na maana ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.
Wanazuoni wengi wanawakosoa al-Ikhwaan al-Muslimuun kwa sababu ya jambo hili. Hawatilii mkazo kulingania kuabudiwa kwa Allaah pekee na kutakasiwa Yeye ´ibaadah na kukemea yale yaliyozuliwa na wajinga pindi wanapowategemea wafu na kuwataka msaada, kuwawekea nadhiri na kuchinja kwa ajili yao, mambo ambayo ndio shirki kubwa.
Jengine wanalowakosoa ni kutoitilia umuhimu kuifuata Sunnah, kuzipa umuhimu Hadiyth tukufu na yale waliyokuwemo Salaf katika hukumu mbalimbali za Shari´ah.
Kuna mambo mengine mengi. Nasikia mengi ambayo al-Ikhwaan wanakosolewa kwayo. Tunamuomba Allaah awaongoze. (al-Majallah (Toleo la 806, uk. 24, 1416-02-25))
Kuna mpingaji mmoja aliyepinga jawabu la ´Allaamah Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na akaonyesha utovu wa nidhamu. Ameandika yafuatayo:
”Mimi nakuheshimu, nakutukuza na nakupenda kwa ajili ya Allaah. Lakini hata hivyo napingana na wewe. Hii leo nimesoma katika ”al-Majallah” maneno yako kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun yanayonasibishwa kwako. Mwandishi ameandika kuwa al-Ikhwaan al-Muslimuun hawatilii umuhimu ´Aqiydah, wanasherehekea mazazi maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba wanafanya lukuki ya Bid´ah. Nilishangazwa sana na maneno haya. Kwa sababu mimi nimefanya kazi na al-Ikhwaan al-Muslimuun huko Misri kwa miaka mingi na sitambui chochote katika hayo. Katika matangamano yangu sikuona kwao Bid´ah yoyote wala chochote katika yale yaliyotajwa katika makala hii. Kwa ajili hiyo nataraji kuwa utarekebisha maneno haya.”
Allaah ni mkubwa! Anamtaka Shaykh ayarekebishe maneno yake aliyoyasema kwa elimu na utambuzi. Je, Imaam Ibn Baaz anazungumza asichokijua? Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Ndipo Shaykh na imaam wa Ahl-us-Sunnah akajibu yafuatayo:
”Ndio, wengi wanasema hivo kuhusu al-Ikhwaan. Mimi nimewanukuu wanazuoni wengi na ndugu kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun kwamba hawatilii umuhimu sana na yenye nguvu katika kutahadharisha yanayohusiana na shirki na ulinganizi wa kuyaomba makaburi. Kwa hali yoyote haya yanaonekana katika vitabu na maisha yao. Ambaye atarejea katika vitabu vyao atayaona hayo.” (Kutoka katika kanda iliyorekodiwa at-Twaa’if, Swafar 1416)
Utaona kuwa muulizaji huyu licha ya utovu wa adabu alionao amekusanya kumsemea uwongo na uzushi Shaykh. Mosi ni utangulizi wake uliopo katika swali:
”Mimi nakuheshimu, nakutukuza na nakupenda kwa ajili ya Allaah.”
Ni nani anayemzungumzisha namna hii? Ni mmoja katika maimamu wa Ahl-us-Sunnah ambaye ameinusuru Sunnah na kuzisambaratisha Bid´ah.
Pili anasema:
”Lakini hata hivyo napingana na wewe. Hii leo nimesoma katika ”al-Majallah” maneno yako kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun yanayonasibishwa kwako.”
Ni utovu wa adabu. Ni kana kwamba muulizaji hajasoma ni vipi mwanafunzi anatakiwa kuwa mbele ya waalimu wake, hajasoma ni namna gani Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) alikuwa akifanya adabu kwa mwalimu wake Imaam Maalik bin Anas au namna ambavyo Imaam Ahmad bin Hanbal alikuwa akifanya adabu na mwalimu wake Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahumu Allaah). Ni bora kwa muulizaji huyu na mfano wake wajifunze adabu na maadili kabla ya kuanza kutafuta elimu. Anasema:
”… maneno yako kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun yanayonasibishwa kwako.”
Hii maana yake ni kuwa imamu (Rahimahu Allaah) ni mwenye kughafilika kwa sababu kinachopata kufahamika katika swali ni kuwa kunaandikwa juu yake yale asiyoyaitakidi au asiyoyajua. Usisahau tena kuwa haya yalikuwa ni mahojiano ya kiserikali na makala yenye umuhumu ambayo mwandishi wa khabari hawezi kuyabadilisha. Na endapo lingetokea hilo basi kamwe Shaykh asingeyanyamazia na khaswa kwa kuzingatia kuwa Shaykh alikuwa anatenga wakati kusoma yanayoendelea katika magazeti.
Tatu anasema:
”Mwandishi ameandika kuwa wanasherehekea mazazi maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba wanafanya lukuki ya Bid´ah.”
Hapa anaendelea kufanya utovu wa adabu kwa Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) pale aliposema: ”Mwandishi ameandika… ”. Hapa anazidi kumsemea uwongo Shaykh pale anapomtuhumu kwamba amesema kuwa wanasherekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanafanya lukuki ya Bid´ah.
Makala ya Shaykh juu ya al-Ikhwaan al-Muslimuun iliyomfanya muulizaji na mfano wake wakasirike ni nakala ya asili. Msomaji sio mjinga anayedanganywa. Soma makala na rejea katika ile asili. Ni wapi imeandikwa kuwa wanahuisha mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanafanya lukuki ya Bid´ah? Lakini kilichopofoka ni macho ni utambuzi wa kuikubali haki na uongofu. Tunamuomba Allaah usalama! Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mtu hatoacha kusema uwongo na kuendelea kusema uwongo mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mwongo.” (Muslim (2607))
Nne muulizaji anasema:
”Nilishangazwa sana na maneno haya. Kwa sababu mimi nimefanya kazi na al-Ikhwaan al-Muslimuun huko Misri kwa miaka mingi na sitambui chochote katika hayo.”
Namuomba Allaah mshangaaji huyu asome vitabu vya pote hilo, kama alivomuashiria imamu mwishoni mwa swali lake. Ikiwa huwezi kusoma kutokana na ufinyu wa wakati wako, basi rejea kurasa za kabla yake. Hapo utayaona kwa kifupi yale wanayoyafanya al-Ikhwaan al-Muslimuun juu ya kiongozi wao Hasan al-Bannaa. Yale usiyoyajua basi utambuzi wao unakutosheleza.
Ungetambua kanuni isemayo ”Yule ambaye amehifadhi atangulizwa mbele ya yule ambaye hakuhifadhi”, ”Ukosoaji unatangulizwa mbele ya usifiaji” na ”Ziada ya mwenye kuaminika ni yenye kukubaliwa” na kwamba mzungumzaji ni kiongozi wa kujeruhi na kusifia katika wakati wake na kwamba hajeruhi na wala hasifii isipokuwa mpaka ahakikishe, basi usingeingi katika uliyoingia.
Tano anasema:
”Katika matangamano yangu sikuona kwao Bid´ah yoyote wala chochote katika yale yaliyotajwa katika makala hii. Kwa ajili hiyo nataraji kuwa utarekebisha maneno haya.”
Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Ni ujasiri ulioje wa kipumbavu na mashambulizi haya juu ya mlima huu! Anamtaka mtu ambaye ndiye marejeo ya ummah katika zama zake apinde kutokana na haki. Naapa kwa Allaah kwamba mimi nawatambua wanazuoni watukufu katika marafiki zake (Rahimahu Allaah) ya kwamba walikuwa wakiona hayaa kusimama na kuzungumza mbele yake msikitini au katika kikao alipo mpaka wamuombe idhini au awape idhini. Miongoni mwao wako ambao walikuwa ni wajumbe katika baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´. Mtu aseme nini juu ya kutaka matakwa kama haya?
Sita imamu (Rahimahu Allaah) ametoa jawabu la kuponda pale alipotilia mkazo yale aliyoyasema katika makala yake iliyotangulia na akamwongozea muulizaji na mfano wake kwamba arejee vitabu vya kipote hiki ili kuhakikisha yale yaliyosemwa.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 119-125
- Imechapishwa: 27/02/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 119-125
Imechapishwa: 27/02/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/40-je-ulinganizi-wa-shaykh-muhammad-bin-abdil-wahhaab-ni-ulinganizi-wa-kiislamu-wa-kivyamavyama-kama-vile-ulinganizi-wa-al-ikhwaan-al-muslimuun-na-wa-jamaaat-ut-tabliygh/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)