Wakati mwanamke anataka kutoka nyumbani na mume amesafiri

Swali: Kumetokea magomvi kati yangu na mume wangu. Anasafiri na ninapotaka kutoka nje ya nyumba inabidi ima nimpigie simu au nimtumie ujumbe, lakini haitikii. Je, nikitoka pasi na idhini yake nakuwa ni mwenye kutenda dhambi kwa sababu safari yake inakuwa ndefu?

Jibu: Usitoke bila ya idhini yake. Haitoshi kumjulisha peke yake, ni lazima atoe idhini. Isipokuwa ikiwa kama kuna hitajio la dharurah ambalo unalihitaji wakati anapokuwa mbali nawe na hakuna yeyote awezaye kukutimizia halo. Katika hali hiyo utatoka kwa kiasi cha hitajio hilo unalotaka pamoja na kujisitiri, kujiheshimu na kufupisha muda kadri na itakavyowezekana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
  • Imechapishwa: 27/02/2024