Swali: Ni kwa nini imeitwa Tarawiyh? Ni upi msingi wa swalah hiyo?

Jibu: Inasemekana kwamba walikuwa wakipumzika (يرتاحون) baada ya kila Rak´ah mbili kutokana na urefu wa kusimama.

Msingi wake ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu katika zile nyusiku za mwanzo. Msikiti ukajaa waswaliji. Usiku wa tatu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutoka nje kwa kuchelea swalah hiyo isije kufaradhishwa kwao. Baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ndipo ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akawakusanya nyuma ya imamu mmoja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 01/04/2022