Katika Hadiyth na mapokezi haya sehemu kubwa inahusiana na mtoto anayekufa kabla ya kubaleghe. Lakini hata hivyo wazazi huhisi msiba, huzuni na masikitiko makubwa pindi mtoto wao ambaye kishainukia na mwema akifa kuliko mtoto wao mdogo. Hili khaswa pale ambapo mtoto akiwa amebobea katika elimu, mwenye kuwatendea wema wazazi, ndugu na marafiki au ana sifa nzuri na matendo yenye kupendeza. Vipi mtoto mdogo anaweza kulinganishwa na mkubwa kwa kuzingatia yale manufaa wanayonufaika kwake wazazi wake na wengineo ikiwa mtoto huyo mkubwa ni mwenye sifa hizo zilizotajwa? Mwenye busara hatakuwa na shaka kwamba huzuni utakuwa mkubwa baada ya yule mtoto mkubwa kutoweka? Katika hali hiyo vilevile ujira utakuwa mkubwa na mwingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 82
  • Imechapishwa: 14/10/2016