42. Kisomo cha Qur-aan katika swalah ya jeneza

10- Swalah ya jeneza

Sunnah ni kusoma “al-Faatihah”[1] na Suurah nyingine. Alizisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sauti ya chini baada ya Takbiyr ya kwanza[2].

[1] Haya ni maoni ya Imaam ash-Shaafi´iy, Ahmad, Ishaaq na vilevile wahakiki wengi katika Hanafiyyah waliokuja baadaye. Kuhusu kusoma Suurah baada yake ni maoni ya Shaafi´iyyah na ni sahihi.

[2] an-Nasaa’iy na at-Twahaawiy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 107
  • Imechapishwa: 15/02/2017