Kuna aina mbili ya majina ya Allaah:
1 – Kuna sampuli ambayo ni maalum kwa Allaah na haifai kwa mwengine kujiita nayo. Mfano wa majina hayo ni Allaah. Hili ndio jina tukufu zaidi la Allaah ambalo haifai akajiita nalo mwengine. Vivyo hivyo Mwingi wa rehema (ar-Rahmaan) haiwezekani kwa yeyote akajiita ar-Rahmaan. Vilevile Mola wa walimwegu, Mfalme wa wafalme, Muumba wa viumbe, Mwenye kunufaisha, Mwenye kudhuru, Mwenye kutoa (al-Mu´twiy), Mwenye kuzuia (al-Maaniy´), Mwenye kukamata (al-Qabdhw), Mwenye kukunjua (al-Baasitw), Mwenye kushusha (al-Khaafidhw) na Mwenye kunyanyua (ar-Raafiy´).
2 – Kuna sampuli ambayo ni majina ambayo Allaah anashirikiana kuitwa nayo na viumbe. Mfano wa majina hayo ni (Mwenye huruma) ar-Rahiym. Hili ni jina shirikishi. Anaitwa nalo Allaah na wengineo. Amesema (Ta´ala) kuhusu Mtume wake:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
”Hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni na kwa waliomuamini ni mpole na mwenye huruma.”[1]
Amemsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni mwenye huruma. Mengine ni kama Mwenye nguvu asiyeshindika (al-´Aziyz), Muweza (al-Qadiyr), Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
Kila jina miongoni mwa majina ya Allaah kunatolewa ndani yake sifa. Sio majina matupu. Bali yamebeba sifa. Mwingi wa huruma (ar-Rahiym) limebeba sifa ya huruma. Mjuzi wa kila kitu (´Aliym) limebeba sifa ya ujuzi. Muweza (Qadiyr) limebeba sifa ya uwezo. Mwenye kusikia kila kitu (as-Samiy´) limebeba sifa ya usikizi. Mwenye kuona kila kitu (al-Baswiyr) limebeba sifa ya kuona. Mwenye hekima (al-Hakiym) limebeba sifa ya hekima. Mtukufu (al-´Adhwiym) limebeba sifa ya utukufu na mengineyo.
[1] 09:128
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 70-71
- Imechapishwa: 13/06/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
21. Sampuli mbili ya majina ya Allaah
Majina ya Allaah ni aina mbili: 1 – Aina ya majina ambayo ni maalum kwa Allaah. Haifai kumwita kwayo mwingine. Mfano wa majina hayo ni Allaah, Mola wa walimwengu, Muumbaji wa viumbe, Mfalme wa wafalme, Mwenye kuchukua (القابض), Mwenye kukunjua (الباسط), Mwenye kushusha (الخافض), Mwenye kunyanyua (الرافع), Mwenye kunufaisha, Mwenye…
In "Sharh Usuwl-ith-Thalaathah - ar-Raajihiy"
Majina maalum kwa Allaah ambayo haifai kwa viumbe kuitwa nayo
Swali: Je, kuna majina ambayo haifai kuitwa kwayo? Jibu: Haifai kuitwa kwa majina ambayo ni maalum kwa Allaah kama vile ´Allaah`, ´ar-Rahmaan` (Mwingi wa huruma), ´Maalik-ul-Mulk` (Mfalme wa wafalme), ´Khaaliq-ul-Khalq` (Muumba wa viumbe), ´Rabb-ul-´Aalamiyn” (Mola wa walimwengu), ´an-Naafiy´ adh-Dhwaar` (Mwenye kunufaisha, kudhuru), ´al-Mu´twiy al-Maaniy´` (Mwenye kutoa, Mwenye kuzuia), ´Haakim-ul-Hukkaam` (Hakimu…
In "Uchaguzi wa majina ya watoto"
25. Aina ya pili majina ya haramu
2- Majina ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Haijuzu kutoa jina kwa jina ambalo ni maalum kwa Mola (Subhaanahu wa Ta´ala). Mfano wa majina hayo ni ar-Rahmaan, ar-Rahiym, al-Khaaliq na al-Baariy. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha majina ya sampuli hiyo. Katika Qur-aan tukufu: هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا "Je, unamjua…
In "Tasmiyat-ul-Mawluud"